Kwa ufupi
Inadaiwa kuwa nyaraka hizo katika Ofisi ya AG,
mkoani Mara, zilighushiwa na askari kanzu mmoja wa Kituo cha Mugumu,
ambaye alikuwa akitumiwa na kamanda aliyeondolewa kusaidia mtandao huo,
pamoja na mtumishi mmoja wa ofisi hiyo (majina tunayahifadhi kwa sasa).
GP Said Mwema.
GP Said Mwema.
POLISI wametajwa kuwa miongoni mwa taasisi za dola ambazo
zimekuwa zikisaidia kukua kwa vitendo vya ujangili katika hifadhi za
taifa, mapori ya akiba na maeneo mengine.
Katika tukio la karibuni, polisi katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, wanadaiwa kwamba walighushi nyaraka za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuziwasilisha mahakamani kwa lengo la kuwaachia huru watuhumiwa waliokuwa na kesi ya kukutwa na silaha kinyume cha sheria.
Katika tukio la karibuni, polisi katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, wanadaiwa kwamba walighushi nyaraka za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuziwasilisha mahakamani kwa lengo la kuwaachia huru watuhumiwa waliokuwa na kesi ya kukutwa na silaha kinyume cha sheria.
Watuhumiwa hao ni wale wanaodaiwa kutumia silaha
hizo kwa kufanya uwindaji haramu kwenye mbuga za wanyama kinyume cha
sheria, huku mtandao mkubwa walionao katika vyombo vya dola ukichangia
vitendo hivyo kuendelea.
Jana gazeti hili lilifichua namna ambavyo baadhi
ya mahakimu wamekuwa wakishiriki katika kufanikisha ujangili na biashara
ya meno ya tembo na nyara nyingine za Serikali kwa kuwapa watuhumiwa
wanaofikishwa mahakanani dhamana na baadaye watuhumiwa hao hutoweka.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili ulibaini kuwa
baadhi ya watuhumiwa, ambao wamewahi kunaswa na kufikishwa mahakamani
kwa tuhuma za ujangili, wametoweka katika njia za kutatanisha na kuacha
kesi zikiendelea huku taarifa zikifikishwa mahakamani kwamba watuhumiwa
hao wamefariki dunia.
Hata hivyo, mmoja wa watuhumiwa hao Malango Dusara
aliyeripotiwa kufariki, anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 3
ya 2010, mkoani Shinyanga kwa kukutwa na risasi 548, amekamatwa tena na
sasa yuko mahabusu, baada ya kukutwa akiishi mitaani.
Wakati hayo yakiendelea katika mkondo wa mahakama,
baadhi ya polisi wanadaiwa kushiriki uovu huo kwa kuharibu ushahidi wa
kesi za watuhumiwa.
Imebainika kwamba, kuharibiwa kwa kesi hizo
huanzia kwa polisi, ambao wanaandaa mashtaka na hatimaye mahakamani,
ambako inadaiwa watuhumiwa huachiwa na wakati mwingine, hukamatwa tena
kwa makosa yaleyale wakiwa nje ya dhamana, lakini bado huachiwa tena.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa watuhumiwa
wa ujangili akiwamo aliyewahi kutajwa na watuhumiwa wengine kuwa
mfadhili wao kutoka Kibondo, mkoani Kigoma, walifutiwa makosa katika
mazingira yanayohusishwa na rushwa.
Watuhumiwa hao sita wakazi wa Kigoma, Geita na
Tabora ambao walikamatwa katika Kijiji cha Mbirikiri, wilayani
Serengeti, mkoani Mara, Mei 12 mwaka huu, wakiwa na bunduki nne za
kivita aina ya SMG na risasi 436.
Watuhumiwa hao ambao baadaye walifikishwa
mahakamani majina tumeyahifadhi, ambapo baada ya kukamatwa walikabidhi
silaha ambazo ni SMG mbili walizokuwa wamezificha eneo la Usinge,
Tabora na nyingine mkoani Kigoma na kumtaja
mfadhili wao, anayewapa silaha (jina tunalo) ambaye ni mfanyabiashara na
mkazi wa Busunzu Kibondo waliyedai anasambaza vijana hifadhi zote za
Taifa kwa ajili ya kuua tembo na faru.
Mchakato wa mashtaka
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa baada ya kukamatwa mfanyabiashara huyo, kuliibua mvutano baina ya polisi wa mkoani Kigoma na wale wa Mara, ambao walikuwa wakitaka afikishwe Serengeti alikotajwa kwamba anafadhili ujangili, huku wale wa Kigoma wakipinga kwa sababu zisizofahamika.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa baada ya kukamatwa mfanyabiashara huyo, kuliibua mvutano baina ya polisi wa mkoani Kigoma na wale wa Mara, ambao walikuwa wakitaka afikishwe Serengeti alikotajwa kwamba anafadhili ujangili, huku wale wa Kigoma wakipinga kwa sababu zisizofahamika.
0 comments:
Post a Comment