BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS OBAMA KUWALIWAZA FAMILIA YA NEWTOWN ILIYOPOTEZA WATOTO 20 KWA KUPIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA..

 
  Mourners grieve at one of the makeshift memorials for victims of the Sandy Hook Elementary School shooting, December 16, 2012, in Newtown, Conn. 
 A memorial is seen along the road to Sandy Hook Elementary School a day after a mass shooting in Newtown, Connecticut, December 15, 2012.

RAIS wa Marekani Barack Obama Jumapili atakwenda Newtown, jimbo la Connecticut  kuliwaza  wakazi wa mji uliokumbwa na msiba mkubwa baada ya mshambuliaji kuuwa watoto 20 wa shule ya Sandy Hook  pamoja na watu wazima sita.

White House imesema rais Obama  atakutana na familia za waliopoteza wapendwa wao na pia kuwashukuru wote waliokwenda shuleni humo kusaidia waathiriwa wa mkasa huo. 
Bw. Obama  atazungumza  Jumapili jioni kwenye  mkusanyiko wa watu wanaomboleza  pamoja na familia za waathiriwa.

Polisi wa Connecticut wamewatambulisha waliouawa  wakiwemo wasichana 12 na wavulana wanane  wote wa kati ya umri wa miaka 6 na 7.Watu wazima wote sita waliouawa walikuwa wanawake.

Afisa wa afya aliyekagua maiti zao alisema wote walipigwa risasi wakiwa hatua chache kutoka kwa muuaji huyo kabla hajajiuwa kwa risasi.  
Msiba huu wa kihistoria Marekani umegonga vichwa vya habari Marekani na nchi za Ulaya na bara Asia.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: