LEO tunapoadhimisha miaka 51 ya uhuru wa Tanganyika, Watanzania wa kada mbalimbali wanakitazama kipindi hicho kwa namna tofauti, kama wanavyoeleza katika mahojiano haya yaliyofanywa na Elias Msuya. Endelea…
Frank Moyo
NDANI ya miaka 51 ya uhuru, kuna mambo mengi ya maendeleo yamefanyika. Kwa mfano, kuna ajira nyingi, rasmi na zisizokuwa rasmi, zimejitokeza. Wakati huu vijana wengi tumejiajiri kwenye usafiri wa bajaj, hii inasaidia kujikimu kimaisha.
Siyo kwamba tunapata fedha nyingi, lakini tunaweza kujikimu tu kimaisha.
Hata hivyo naweza kusema kuwa bado nchi yetu haijaendelea kama zilivyo nchi za wenzetu.
Wenzetu wana treni zinazopita chini ya ardhi, wana barabara za angani (flyovers). Sisi bado reli na barabara ni zile zile tu.

Nashauri Serikali iwaangalie na wananchi walio
katika ajira zisizo rasmi kwa kuwa ndiyo wengi kuliko watumishi wa umma
na wafanyakazi walio katika sekta rasmi.
Serikali pia iimarishe miundombinu kama reli na barabara ili kuongeza maendeleo.

Japhet Kanyika
SAWA tumepata uhuru, lakini ni wa maneno tu. Hakuna uwajibikaji wa kweli wa kuleta maendeleo.

Kwa mfano elimu yetu tangu tumepata uhuru bado
haijazaa matunda katika jamii. Watanzania wengi hawana elimu ya
kuwawezesha kueleza kero zao, ukilinganisha na raia wa Kenya ambao
wanajua haki zao kwetu bado.
Utakuta mtu hajui hata haki zake au anashindwa kueleza shida yake, mwisho anabaki na umasikini wake.

Kwa upande mwingine, ukiangalia maeneo ya
vijijini, vijana wengi wamejiajiri kwenye biashara ya bodaboda, lakini
hawana mafunzo ya kutosha ya biashara hiyo.
Isitoshe Serikali inaweka ukiritimba kwa vijana, mfano kijana akihitaji leseni ambayo gharama yake ni Sh40, 000 tu, atazungushwa hadi anajikuta ametoa Sh200, 000.

Kwa upande wa kilimo, mimi ni mkulima natoka
wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Wakulima wengi hawana elimu ya kilimo, matokeo yake wanalima mashamba makubwa bila utaalamu, hivyo kuishia kupata mazao kiduchu. Wanatumia nguvu na fedha nyingi lakini hakuna cha zaidi wanachopata.
Nashauri Serikali iwekeze kwenye elimu ili wananchi wajikwamue kiuchumi.

David William
MIAKA 51 ya uhuru, bado hatuna la kujivunia kwa sababu vijana wengi hatuna ajira. Ukiacha vijana waliosoma hadi vyuo vikuu, lakini wengi wetu hatuna cha kufanya, tumebaki na umasikini mtupu.

Mimi ni mwanamichezo na nimechezea timu za
Kombaini ya Makuburi na Simba ‘B’, lakini nimeshindwa kuendelea kwa
sababu ya mazingira magumu. Sina uwezo wa kujikimu kimaisha wala
kujikita kikamilifu kwenye michezo.
Hilo ndio tatizo linalotukumba sisi vijana.
Naamini kabisa kwa kipaji changu hiki cha michezo ningefika mbali, lakini kwa umasikini huu nimeshindwa.

Serikali haina mkakati wowote wa kutukwamua vijana, ndiyo maana sioni faida za kusheherekea uhuru.
Kwa sasa najishughulisha na biashara ya taxi ili kujikimu kimaisha hata kama ndoto yangu ya kuwa mwanamichezo imepotea.

Naishauri Serikali iwekeze kwenye michezo kwa
kutambua vipaji vya vijana na kuviendeleza. Waanzishe shule za soka na
michezo mingine.
Huko ndiko tutakapotokea, siyo lazima vijana wote tukae ofisini, hata huku mitaani tunaweza kujikwamua. Kwa nchi za wenzetu wanamichezo wanalipwa vizuri kuliko hata maofisa wa Serikali.

Saleh Mpiga
NI kweli katika miaka hii 51 ya uhuru kuna mafanikio mengi yaliyopatikana. Uchumi umekua, kilimo kimeimarika, barabara zimejengwa na miundombinu mingine, ukilinganisha na miaka ya nyuma.

0 comments:
Post a Comment