Kituo cha mabasi Ubungo.
WAKATI abiria wanaendelea kulalamikia kupanda kwa nauli za mabasi yaendayo mikoani, hali ya usafiri katika Kituo Kikuu cha mabasi Ubungo imezidi kuwa mbaya.
Hali hiyo imekuja kutokana na kuwapo kwa abiria waliokwama kuelekea mikoa ya kaskazini na nyanda za juu kusini kutokana na uchache wa mabasi.
Mwananchi lilishuhudia abiria wakiwa wamekwama kituoni hapo bila ya kupata ufumbuzi kuhusu safari zao huku wakiwatupia lawama wamiliki wa mabasi, kuwa ndio chanzo cha usumbufu wanaoupata.
Walidai kuwa wamiliki hao wamekuwa wakifanya makosa na hatimaye kufungiwa kwa kampuni zao hali inayosababisha kuwapo kwa uhaba wa mabasi.
Wakizungumzia usumbufu huo, baadhi ya abiria walisema hali hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa abiria wengi wanaokwenda mikoani kwa ajili ya sherehe za mwisho wa mwaka.
“Sisi tuko hapa kituoni tangu asubuhi na bado hatujapata uhakika wa safari kwani abiria ni wengi, ikichangiwa na uhaba wa magari uliojitokeza kwa sasa, tunapata usumbufu wa kuja kituoni na kurudi nyumbani,” alisema mmoja wa abiria hao.
Abiria huyo aliyetajitambuliasha kwa jina moja la Jesca alidai kuwa baadhi ya kampuni zinazomiliki mabasi hayo, zimekuwa zikifanya makosa ya mara kwa mara ambayo yanaweza kuepukika na matokeo yake, wanajikuta wakifungiwa kutoa huduma.
“Kuna makosa mengine yasiyo ya lazima ambayo yanaweza kuepukika ni vyema kampuni miliki zikachukua tahadahari napema ili kuepuka adha unayo tukumba,” alisema Bibi Jesca
Abiria waliokwama katika kituo hiko ni wale wanosafiri kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mikoa ya Tanga, Moshi, Arusha na mikoa ya Iringa na Mbeya.
Abiria waliokwama katika kituo hiko ni wale wanosafiri kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mikoa ya Tanga, Moshi, Arusha na mikoa ya Iringa na Mbeya.
0 comments:
Post a Comment