WAASI WAENDELEA KUTEKA MIJI MINGENE AFRIKA YA KATI.
MUUNGANO mpya wa waasi katika jamhuri ya Afrika ya kati ulianzisha mashambulizi yake upande wa kaskazini mwa nchini Desemba 10.
Kundi hilo la waasi lijulikanalo kama Seleka liliteka mji wa Kaga- Bandoro Jumanne. Waasi hao sasa wako kilometa 300 kutoka mji mkuu Bangui, ulio karibu na kusini mwa mpaka na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Seleka inaunganisha makundi manne ya waasi kutoka kaskazini. Wapiganaji wengi walihusishwa katika mzozo wa miaka minne ambao ulimalizika rasmi kwa mkataba wa amani wa mwaka 2007, licha ya kwamba mapigano yamekuwa yakirudia mara kwa mara upande wa kaskazini tangu mwaka 2009.
Kasi na urahisi ambao jeshi hilo la muungano wa waasi limeweza kuchukua miji muhimu kaskazini inaleta wasiwasi. Wachambuzi wanasema majeshi ya serikali yanatoa upinzani mdogo.Rais wa Afrika ya kati Francois Bozize.
Chad, mshirika wa karibu wa rais Francoise Bozize wamepeleka majeshi kumlinda.
Mkurugenzi wa Afrika ya kati wa shirika la kimataifa la mizozo Thierry Vircoulon amesema jeshi la Chad ndio ngao ya serikali na si rahisi kwa waasi kupambana nao.
Anasema jeshi la Chad limepelekwa kimkakati kwenye maeneo ya mji mkuu ili kuulinda .
Anasema waasi wanadhibiti kiasi cha robo tatu ya mji, hata hivyo lengo si kuchukua Bangui na kuiangusha serikali. Amesema waasi wamechukua miji muhimu ili kuonyesha nguvu zao na kujiweka kwenye nafasi nzuri katika meza ya mazungumzo.
Kutekwa kwa Kanga Bandoro Jumanne kumekuja siku moja tu baada ya waasi kukubali kusitisha kusonga mbele na kuanza mazungumzo.
Serikali imesema haitafanya mazungumzo mpaka waasi hao waondoke kwenye miji waliyoiteka.
Viongozi wa kikanda sita walijiunga chini ya jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya kati wamesema lazima waasi waondoke na wametoa wito wa kufanya mazungumzo ya amani katika mji mkuu wa Gabon Libreville.
Seleka anasema serikali haikuheshimu mikataba ya amani ya mwaka 2007 na 2011 ikiwa ni pamoja na kipengele cha kuwalipa wapiganaji waasi na kuwaingiza kwenye jeshi la serikali.
Maelfu ya waasi wameripotiwa kukimbia mapigano ya hivi karibuni kaskazini ambapo usalama mdogo umekuwa tatizo linalokuwepo na kuondoka.
Msemaji wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu wa Jamhuri ya Afrika ya kati Vincent Pouget ameiambia VOA kwamba mapigano yamekata mawasiliano ya simu za mkononi kwenye eneo hilo.
Anasema ni ngumu kujua ni kiasi gani hasa raia waliokimbia na wapi walipo, jambo linalopelekea juhudi za uokozi kuwa ngumu zaidi .
Amesema baadhi wanakimbia kwenye makazi ya muda mfupi karibu na viwanja hivyo, wakati wengine wanakimbilia maporini, vijiji vya karibu au kwenye maeneo yanayokubalika kama kwenye mishen za kanisa katoliki.
Amesema kuwapatia maji safi ya kunywa na vyoo ni jambo muhimu kuzuia ugonjwa.
Doctors Without Borders wanasema wamepata ripoti za ghasia dhidi ya raia ikiwa ni pamoja na uporaji. MSF inasema wengi wa waliokimbia bado wanaogopa kurudi nyumbani.
0 comments:
Post a Comment