BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAFUASI NA WAPINZANI WA RAIS MORSI WATANGWANA CAIRO


Wafuasi wa Morsi wakimshambulia mpinzani wao.

Wafuasi na wapinzani wa rais wa Misri Mohamed Morsi walipambana Jumanne usiku huko Cairo kwa mawe na mabomu,  wakati washauri wakuu  watatu wa rais huyo wakijiuzulu  kupinga jinsi anavyoendesha mzozo wa kikatiba wa nchi hiyo.

Akiripoti kutoka  Cairo mwandishi wa VOA Elizabeth Arrot amesema ghasia hizo mpya ziliibuka wakati wafuasi wa kiislam wa Morsi waliposhambulia waandamanaji wakipinga kile walichokiita unyakuzi wa  madaraka wa rais Morsi.


Rais wa Misri Mohammed Morsi.

Arrott anasema wafuasi wengi  wa rais walikuwa wanaume wenye madevu wakionekana kuwa moja kwa moja ni wafuasi wa Muslim Brotherhood ambao walishambulia waandishi wa habari nje ya jumba la rais.

Wakati huo huo washauri wengine watatu wa rais walitangaza kujiuzulu wakipinga amri ya rais kujipa madaraka zaidi .Watano kati ya washauri wa rais 17 wamejiuzulu tangu Novemba 22.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: