BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WALIMU WATANGAZA KUHUJUMU WANAFUNZI

Wasambaziana ujumbe kupitia simu za mikononi
*Wengine waacha masomo wakimbia kuendesha bodaboda
*RC awashtukia, asema wanadidimiza elimu 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti 

WALIMU mkoani Simiyu, wamejipanga kuwahujumu wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, baada ya kuanza kusambaziana ujumbe mfupi wa simu za mkononi, wakihamasishana kufanya hivyo kila wanapoingia madarasani.

Taarifa hiyo, ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti alipokuwa akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru.

Kwa mujibu wa Mabiti, ujumbe huo ni hatari kwa kuwa unaweza kusababisha matokeo ya wanafunzi wa sekondari na shule za msingi, kuwa mabaya baada ya kupotoshwa na walimu wao.

“Nasikitika sana kwa vitendo vya baadhi ya walimu ndani ya mkoa huu, kueneza ujumbe wa maandishi kwa njia ya simu za kiganjani, ambao unawahamasisha walimu wawakoseshe wanafunzi wao.

“Ujumbe huu unasomeka hivi, Mchina si mjinga kutengeneza vitu feki, sisi walimu wa Tanzania kwa sababu Serikali haitaki kutulipa vizuri na sisi tutengeneze wanafunzi feki,” ulisomeka ujumbe huo.

Alisema kutokana na ujumbe huo, hatashangaa hata kama matokeo ya darasa la saba na kidato cha nne yakiwa mabaya, kwa kuwa walimu hao walikuwa tayari wameshaanza kupeana taarifa za kupotosha wanafunzi tangu mapema.

Alisema tabia hiyo ya walimu, si njia sahihi ya kudai haki zao, bali kuwajibika na kuwa waadilifu kazini ndiyo njia sahihi ya kufikia malengo yao.

Hata hivyo, alisisitiza suala la maendeleo katika mkoa huo kupitia sekta mbalimbali, ambapo kipaumbele cha kwanza ni kilimo na ufugaji kwa kutoa elimu ya kilimo bora na ufugaji kwa wakulima, ili waweze kuwa na maendeleo na kunufaika zaidi.

Aliwataka wakulima kuhakikisha kila kaya inalima ekari mbili za mtama na kwamba hilo ni agizo na ili kuhakikisha kwamba kaya inatekeleza hilo, ekari hizo zitakaguliwa na wataalamu wa kilimo.

Wakati huo huo, aliwaonya watumishi wa Serikali mkoani hapa, wasijihusishe na biashara wakati wa kazi ikiwamo kuendesha bodaboda na atakayekiuka utaratibu huo, atachukuliwa hatua za kinidhamu.

Pamoja na mambo mengine, Mabiti aliyasema hayo kutokana na baadhi ya watumishi wa Serikali wakiwamo walimu wa shule za msingi na sekondari, kufanya biashara ya bodaboda wakati wa kazi na kuacha kufundisha wanafunzi.

Ili kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa, mkuu huyo wa mkoa alimuagiza Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, kuhakikisha walimu na watumishi wote wa Serikali watakaokuwa wakifanya biashara wakati wa kazi, wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Aliwataka walimu wakuu na wakuu wa shule, kuhakikisha wanasimamia maendeleo ya walimu wao katika ufundishaji, kwa kuwa wao ndio wakaguzi wa kwanza.

“Nyie walimu wakuu na wakuu wa shule, nitaanza kwanza kuwawajibisha nyinyi kabla ya wengine na kama mmeshindwa kazi andikeni barua mjiuzulu mapema.

“Atakayejaribu kufanya mzaha katika hili, atanichukia, sitakuwa na huruma kwa mtumishi yeyote yule anayefanya uzembe kazini, hata kauli mbiu ya maadhimisho haya inasisitiza uadilifu na uwajibikaji kazini,” alisema Mabiti.

Pia alisisitiza suala la maendeleo katika mkoa huo kupitia sekta mbalimbali na kusema, kipaumbele cha kwanza ni kilimo na ufugaji na ili hilo liweze kufanikiwa, lazima itolewe elimu ya kilimo bora na ufugaji kwa wakulima, ili waweze kuwa na maendeleo na kunufaika zaidi.

Aliwataka wakulima kuhakikisha kila kaya inalima ekari mbili za mtama na kwamba hilo ni agizo na ili kuhakikisha kwamba kaya inatekeleza hilo, ekari hizo zitakaguliwa na wataalamu wa kilimo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: