BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ABIRIA WA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPATA AJALI IKIHUSISHA DALADALA IGOMA JIJINI MWANZA.



Askari wa usalama barabarani wakipima ajali iliyotokea jana jioni eneo la Igoma jijini Mwanza na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye anatajwa kuwa ni abiria ambaye alikuwa amembeba dereva wa pikipiki iliyopata ajali yenye namba za usajili T988 BDW ambapo dereva wake (ambaye ndiye mmiliki aliyekuwa amepakizwa) alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea, inasemekana kuwa pikipiki hiyo iliyokuwa kwenye mwendo kasi iligonga kwa nyuma basi la abiria aina ya daladala lenye namba za usajili T768ASA lililosimama ghafla mbele ya pikipiki hiyo kwa ajili ya kupakia abiria.




Pikipiki hiyo yenye namba za usajili T988 BDW eneo lake la mbele limezama kabisa uvunguni mwa daladala kiasi cha kuharibika vibaya.

Baada ya trafiki kufanya upimaji gari la abiria (daladala) linalofanya safari zake Buzuruga hadi Sumve liliruhusiwa kutoka barabarani na kupaki pembeni kwaajili ya taratibu nyingine kufanyika ikiwa ni pamoja na kuuondoa mwili wa kijana huyo pamoja na pikipiki iliyopata ajali ili kupisha shughuli nyingine za usafirishaji barabarani kuendelea. 



Kisha mwili wa marehemu Mayunga Clement Lufuta ukatolewa barabarani kusubiri gari maalum kupelekwa hospitali ya rufaa Bugando kuhifadhiwa.

Kujulikana kwa jina la marehemu huyo kumekuja mara baada ya askari wa usalama barabarani kumpekua na ndipo walipokuta walet yenye vitambulisho mbalimbali kikiwemo kitambulisho cha mpiga kura. 

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: