BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AU, YAOMBA MSAADA KWA NATO JUU YA MALI.


MWENYE wa Muungano wa Afrika, Thomas Boni Yayi, ametoa wito wa kutuma vikosi kusaidia wanajeshi kupambana na makundi ya wapiganaji nchini Mali.

Wapiganaji hao ambao wanajumuisha wale wa Tuareg, wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi.


''Mzozo wa Mali ulikuwa kitendawili cha kimataifa na NATO inapaswa kusaidia kama ilivyo saidia Afrghanistan,'' alisema Thomas Boni Yayi.

''Hata hivyo, harakati dhidi ya wapiganaji hao zinapaswa kuongozwa na kikosi cha Afrika,'' aliongeza kusema bwana Yayi.

Mwezi jana Umoja wa Mataifa uliidhinisha mipango ya kutuma takriban kikosi cha wanajeshi elfu tatu nchini Mali.

''Bila shaka tuna wasiwasi kuhusu hali na hofu ya kuendelea kuwepo makundi ya kigaidi katika eneo hilo , inaleta wasiwasi kwa kila mtu kimataifa''.

Maafisa wa UN wanasema kuwa hawakutarajia wanajeshi hao kutumwa huko kabla ya mwezi Septemba.

Bwana Yayi, ambaye ni rais wa Benin,alitoa wito wake baada ya mazungumzo na waziri mkuu wa Canada Stephen Harper mjini Ottawa.
Wapiganaji wa Tuareg wameteka eneo la Kaskazini mwa Mali
"NATO inapaswa kuchukua jukumu lake katika mzozo huu, na kwamba kikosi cha Afrika kitatoa mwongozo, sawa tu na hali ilivyokuwa nchini Afghanistan,''

Wanachama kadhaa wa NATO ikiwemo, Marekani na Ufaransa, wako tayari,kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Afrika watakaoshiriki katika harakati hizi za kumaliza uasi, ingawa hawajajitolea kutuma vikosi.

Harper alisema kuwa Canada , ambayo ni mwanachama wa , Nato, haijatafakari zaidi kuhusu kujihusisha kijeshi nchini Mali.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: