KWA UFUPI
“Muungano huu umekuwa chachu ya maendeleo kwa Wazanzibari, ndiyo maana Serikali ya Umoja wa Kitaifa itaendelea kuudumisha. Nafahamu kuna changamoto za Muungano, ambazo Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano inazishughulikia. Tunachotakiwa ni kuendelea kuudumisha, ili ushirikiano wetu uzidi kuwa imara kwa faida na maslahi ya Watanzania wote,”![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjtW8_GaTtxSvf2M50Ncdsgav-UhyphenhyphenjOQBDbqxUV9FFXlL9v6abTss61Aba-OsrfWhtVtWryDwl2DA-YKm7HVK4yG0hLq3A-yJUlcJbzA7_tHSvdxggr6KL7y2kAUYwVQ-SpJjiqNKh0c14/s640/IMG_5387.JPG)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wakati alipomaliza kukagua gwaride la Vikosi vya ulinzi katika kilele cha sherehe za kutimiza Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja. Baadhi ya Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zabzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Amani Abeid Karume,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Salmin Amour Juma,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika jan. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein
amesema kuwa Serikali yake na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, zitaendelea
kushirikiana katika kuendeleza na kuulinda muungano ulioipatia sifa Tanzania
kutokana na kuimarika kwake.
Dk Shein aliyasema hayo jana katika maadhimisho ya miaka 49 ya
Mapinduzi Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Aman mjini Zanzibar.
“Muungano wetu upo imara na umepata heshima kubwa sana katika
mataifa mbalimbali, Serikali zetu mbili zitaendelea kushirikiana katika
kuendeleza muungano wetu na kamati za pamoja za kushughulikia kero za muungano,
zitaendelea kuyapatia ufumbuzi yale ambayo wameanza kuyashughulikia,” alisema
Dk Shein.
Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib
Bilali, Dk Shein alisema kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa
mfano wa kuigwa, ndani na nje ya nchi kutokana na mafanikio yaliyofikiwa
kiuchumi na kisiasa.
“Muungano huu umekuwa chachu ya maendeleo kwa Wazanzibari, ndiyo
maana Serikali ya Umoja wa Kitaifa itaendelea kuudumisha.
Nafahamu kuna
changamoto za Muungano, ambazo Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano inazishughulikia. Tunachotakiwa ni kuendelea kuudumisha, ili
ushirikiano wetu uzidi kuwa imara kwa faida na maslahi ya Watanzania wote,”
alisema Dk Shein.
Dk Shein pia aliwakumbusha wananchi umuhimu wa mapinduzi
yaliyotokea Januari 12, 1964, akisema mapinduzi hayo yamerudisha utu na heshima
ya Wazanzibari, ambao sasa wanaishi kwa mshikamano na maelewano.
Dk Shein
aliwataka wananchi wote wa visiwa hivyo kufanya kazi kwa bidii, ili kujiletea
maendeleo kama sehemu ya kumuenzi Mzee Abeid Amani Karume na waasisi wengine wa
mapinduzi hayo.
Alisema kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na wananchi katika shughuli za kimaendeleo ili kujenga uchumi imara wa Zanzibar.
“Tuna changamoto nyingi za kimaendeleo. Vijana wetu wengi hawana
ajira, lakini Serikali itahakikisha inawapatia mikopo na mafunzo kupitia
vikundi vyao, ili waweze kushiriki katika uzalishaji mali.
Pia wajasiriamali
nao tutajitahidi kuwawezesha ili kuongeza tija katika shughuli zao za
kimaendeleo,” alisisitiza Dk Shein.
Mafanikio
ya Serikali
Akizungumzia mafanikio Dk Shein alisema kwamba Serikali yake imepata mafanikio makubwa katika sekta ya afya, elimu na miundombinu, huku akiwahakikishia Wazanzibari kuimarika kwa upatikanaji wa maji na umeme katika kipindi kifupi kijacho.
Akizungumzia mafanikio Dk Shein alisema kwamba Serikali yake imepata mafanikio makubwa katika sekta ya afya, elimu na miundombinu, huku akiwahakikishia Wazanzibari kuimarika kwa upatikanaji wa maji na umeme katika kipindi kifupi kijacho.
Dk Shein alisema ukuaji wa uchumi unatazamiwa kufikia asilimia
saba kutoka asilimia 6.8 katika mwaka 2011, huku pato la taifa likiongezeka kwa
Sh1,198 bilioni katika mwaka 2011 kutoka Sh946.8 bilioni katika mwaka 2010.
Alisema kuwa mafanikio hayo ya kukua kwa uchumi yamesaidia kwa
kiasi kikubwa kushuka kwa mfumuko wa bei wa bidhaa mbalimbali za chakula kutoka
asilimia 20.8 Desemba mwaka 2011, hadi 4.2 Novemba mwaka 2012 na kutoa
faraja kubwa kwa wananchi.
Rais huyo wa Awamu ya Saba wa Zanzibar alisema kuwa ukusanyaji
wa mapato ya ndani umeongezeka kutoka Sh181.4 bilioni mwaka wa fedha 2010-2011
na kufikiya Sh212 bilioni katika mwaka 2011-2012, ikiwa ongezeko la
asilimia 17.
0 comments:
Post a Comment