Kwa ufupi
Wakati hayo yakitokea huko Karatu, mwanamke
mwingine, mkazi wa Kijiji cha Miangalua, wilayani Sumbawanga, Mkoa wa
Rukwa anatuhumiwa kumuua mumewe kwa kumkata mapanga kichwani kwa madai
ya kuuza mahindi sado mbili.
IGP SAID MWEMA.
MAMA mmoja mkazi wa Kijiji cha Rhotia wilayani Karatu,
anashikiliwa na polisi akidaiwa kuwaua watoto wake wawili kwa kuwachinja
kama kuku.
Wakati hayo yakitokea huko Karatu, mwanamke
mwingine, mkazi wa Kijiji cha Miangalua, wilayani Sumbawanga, Mkoa wa
Rukwa anatuhumiwa kumuua mumewe kwa kumkata mapanga kichwani kwa madai
ya kuuza mahindi sado mbili.
Kwa Karatu, hilo ni tukio la pili kubwa la mzazi
kuua wanawe baada ya lile la Mkazi wa Kijiji cha Gekrumu wilayani humo,
Evance Damiani (43), kuwaua watoto wake wanne kisha na yeye kujiua kwa
kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Marehemu Damiani
aliwacharanga kwa shoka watoto wake, Theophil (11), Ritha (9) na pacha
Jigimu na Theodore (6).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas
alithibitisha jana kutokea kwa mauaji ya watoto hao na kueleza kuwa
uchunguzi bado unaendelea.
“Ni kweli tumepata taarifa hizo kutoka Karatu na
uchunguzi wa tukio hilo umeanza ili kujua chanzo cha mama huyo kufanya
mauaji hayo,” alisema Kamanda Sabas.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Rhotia, Andrea Mallu alisema jana kwamba mama huyo aliwaua watoto wake usiku wa kuamkia jana.
Mashuhuda waliwataja watoto hao waliochinjwa kuwa
ni Mariana Juma (9) mwanafunzi wa darasa la tatu na Patrice Juma (6)
anayesoma chekechea.
“Imesemekana kuwa aliwachinja kwa sababu watoto
wake walizuiwa kubatizwa na Jumuiya ya Kikatoliki ya Yohanne Mseyi,”
alisema mmoja wa mashuhuda hao ambaye hakutaka kutaja jina lake
liandikwe gazetini.
Habari zimeeleza kuwa mama huyo sasa anashikiliwa
katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Karatu baada ya kukamatwa na
wanakijiji wenzake.
Mallu alidai kuwa mwanamke huyo aliwachinja watoto
wake hao wakati bibi yao akiwa katika msiba wa nyumba ya jirani na muda
mfupi baada ya kufanya tukio hilo alitoroka.
“Wananchi walishirikiana na kuanza kumsaka na saa
5:00 asubuhi jana walimkuta katika nyumba moja iliyokuwa ikijengwa akiwa
amejificha. Alipohojiwa, hakutaka kusema chochote badala yake alitoa
karatasi yenye ujumbe kuwa amefanya hivyo baada ya wanajumuiya kukataa
kuwabatiza watoto wake.”
Hata hivyo, Mallu alisema kuwa Jumuiya hiyo ya
Yohanne Mseyi imekana madai ya mama huyo ikieleza kuwa hakuwahi kuchukua
hata fomu zilizokuwa zimetolewa kwa ajili ya ubatizo wa watoto.
0 comments:
Post a Comment