Baba mzazi wa marehemu, Baya Kidinga (20), Katambi
Jidiga kulia akimsikiliza Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile kulia akimweleza jambo juu ya tukio la mauaji ya mtoto wake lililotokea januari 26/ 2013 baada ya kudaiwa askari polisi waliokuwa katika zoezi la udhibiti na ufuatilia kumpiga risasi.
Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jidai mkoa wa Morogoro Hamis Seleman kulia akimsihi ndugu wa marehemu,Baya Kidinga (20), Madaha Shirinde baada ya kususia maiti mpaka serikali itimize mashrti yaliyowekwa na familia hiyo ndipo wakulibali kuchukua mwili na kuuzika.
Baba mzazi wa marehemu, Baya Kidinga (20), Katambi
Jidiga (katikati) akibembelezwaa na mtoto wake Madaha Shirime kushoto na afisa mtendaji kijiji cha Ipera Asilia, Zikeni Magoha kulia.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile kushoto akimsikiliza Manogeleku Kisandu kulia ambaye ni shahidi aliyeshuhudia tukio la kupigwa risasi marehemu Baya Kidinga (20) na askari polisi januari 31/ 2013 katika Kitongoji cha Lugangeni Kijiji cha Ipera Asilia
Tarafa ya Mtimbira wilaya ya Ulanga Mkoani hapa.
Sehemu ya wafugaji wa jamii ya wasukuma wakimsikiliza kamanda wa polisi Morogoro (hayupo pichani) wakati wa tukio hilo.
Eneo ambalo linadaiwa marehemu Baya Kidinga (20) alipigwa risasi na kufariki dunia baada ya askari polisi kumfyatulia na kupoteza maisha damu ikiwa imetapakaa chini, picha iliyopigwa januari 27/ 2013.
Marehemu Baya Kidinga (20) enzi za uhai wake.
Kitambulisho cha marehemu Baya Kidinga (20) cha kuhitimu mafunzo ya Mgambo mkoa wa Morogoro.
Sehemu kubwa ya wafugaji wilaya ya Ulanga wakimsubiri mkuu wa wilaya ya Ulanga Francis Miti baada ya familia ya marehemu kukataa kutambua mwili wa marehemu ndugu yao anayedaiwa kupigwa risasi na askari polisi waliokuwa katika zoezi la udhibiti na ufuatilia wa mifugo katika hifadhi ya bonde la mto Kilombero kuupokea na kwenda kuulizika yaliyotolewa na kamanda wa polisi ya mkoa Morogoro huo.
Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Francis Miti kulia akimsikiliza Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile kushoto baada ya kamanda huyo kukataliwa na familia ya marehemu Baya Kidinga (20) kutambua mwili wa marehemu kisha kukubali kuupokea na kwenda kuuzika.
Mkuu wa wilaya ya Ulanga Francis Miti kushoto akizungumza na wafugaji (hawapo pichani) baada ya wafugaji hao kususia maiti kwa siku mbili wakidai mpaka serikali itimize masharti yaliyowekwa na familia. kushoto ni Kamanda wa polisi Morogoro Shilogile na katikati ni Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ulanga Halidi Nalyoto.
HABARI KAMILI HII HAPA.
JESHI la polisi Wilayani
Ulanga Mkoani Morogoro limelazimika kurudisha jumla ya sh 10 milioni
zinazodaiwa kuporwa kwa mfugaji wa jamii ya kisukuma baada ya kumuuwa kwa
kupigwa risasi mdogoni hatua hiyo ilikuja baada ya kususiwa maiti hiyo kwa siku
mbili.
Hatua ya utekelezaji wa
urudishaji wa pesa hizo zilizokuwa zikilalamikiwa na ndugu wa mfugaji huyo aliyefahamika
kwa jina la Baya Katambi Kidiga ni sehemu ya makubaliano yaliofikiwa mbelee ya
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Francis Mitti na Mkuu wa jeshi la polisi Mkoani hapa
Faustine Shilogile, Mkuu wa upelelezi makosa ya jinai mkoani hapa Hamisi
Selemani, Mkuu wa polisi Ulanga.
Sakata hilo la mauaji na
uporaji linaloendelea kulichafua jeshi la polisi Mkoani Morogoro limetokea
tarehe 26, January 2013 katika Kitongoji cha Lugangeni Kijiji cha Ipera Asilia
Tarafa ya Mtimbira wilaya ya Ulanga Mkoani hapa.
Awali polisi hao walidaiwa
kutekeleza mauaji hayo majira ya saa 4 kwa kumpiga risasi marahemu huyo na
kuuchukua mwili wake na kuupeleka kituo cha afya Mtimbira haraka haraka kwa
kutumia gari la polisi linalodaiwa likishiriki katika operationi ya kukamata mifugi
wilayani humo kutoka kwenye hifadhi ya bonde la mto Kilombero.
Baadhi ya masharti ambayo
polisi walitakiwa kutekeleza ni kutoa ripoti ya kina ya uchunguzi wa kifo
kutoka kwa daktari ambao utabainisha kuwa marehemu Baya Kidinga (20) amefariki
dunia kwa kupigwa kwa risasi.
Hatua ambayo jeshi hilo
lilitekeleza kwa kutoa ripoti daktari alitoa riporti ya mauaji hayo
yaliodhibitisha bila shaka kuwa ameuwawa kwa kupigwa risasi ambayo ilikubaliwa.
Sharti la pili ambalo polisi
walitakiwa kutekeleza ni kujua ni kwanini mwili wa marehemu ulihamishwa toka
katika eneo la tukio kwa haraka bila hata kutoa fursa ya ndugu zake kuwepo na
baadhi ya ndugu na majirani waliokuwa waliotaka kufuatilia juu ya mkasa huo walizuiwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro,
Faustine Shilogile alikuwa wa kwanza kuonja makali ya wananchi ambapo aliwasili
majira saa saa 5 asubuhi siku ya tukio na jopo la maafisa wa jeshi hili huku
idadi ya wafugaji wakiendelea kukusanyika kwa kuulizwa maswali yaliomshinda
ikiwemo kutakiwa kueleza kama operationi ya kuwaondoa wafugaji katika hifadhi
ya bonde la mto Kilombero ipo au imekwisha na eneo ambalo marehemu ameuwawa
ndani ya hifadhi ama laa.
Shilogile akijibu maswali
hayo alisema kuwa operationi anachojua yeye ilisitishwa katika wilaya ya
Kilombero lakini kwa wilaya ya Ulanga hilo hatakuwa na jibu la swali hilo
lakini swahili litajibiwa na mkuu wa wilaya ya Ulanga pindi atapofika.
“Poleni kwa msiba huu mimi
nimekuja na timu ya wenzangu akiwemo mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wetu
lakini natumaini kila kitu kitaenda sawa na kingine mimi nimekuja eneo la tukio
kutaka kujua ukweli wa tukio hili ili kubaini ukweli wenyewe ikiwemo nani
amefanya kosa na mpaka sasa askari wetu waliohusika katika tukio hilo tayari
tunawashikilia kwa ajili ya uchunguzi wa awali na wakibaini sheria itachukua
mkondo wake” alisema Shilogile.
Kamanda huyo ambaye
alikabiliwa na maswali mengi kutoka kwa wafugaji hao likimwemo la msemaji wa
familia hiyo ya marehemu, Baya Kidinga (20), (Madaha Shirinde) aliyeuliza kwa
kutaka ufafanuzi wa kina kwa kuuliza swali je askari aliyepata mafunzo anapaswa
kufanya nini pindi anapokabiliana na mtu mwenye silaha za asili ikiwemo fimbo ?
ama kutuliza ghasia au vurugu anapaswa kutumia bunduki kwa kupiga mwananchi
katika eneo gani ?.
Akijibu maswali hayo Kamanda
wa polisi Morogoro, Shilogile alijibu kuwa anapaswa kumpiga mtu risasi kwa
kutumia bunduki kwenye miguu na kueleza kuwa yeye amefika eneo hilo na timu
yake kwa lengo la kujua mazingira ya tukio lililivyofanywa na askari baada ya
kufanya uchunguzi na kuwahoji walioshuhudia.
Majibu hayo ya kamanda
yalizusha mzogo mkali kutoka kwa wananchi hao na kuzalisha maswali mengine
likimo la kuhoji kwanini askari wako ametumia silaha kwa kumpiga marehemu
risasi mdogoni kama amepata mafunzo ?.
Kamanda huyo alieleza tena
kwa umati wa wafugaji hao kwa kusema kuwa kwa wakati huo atakuwa na jibu la
swali hilo na kuongeza hawezi kujua kilichompata askari huyo mpaka ametumia
silaha kwa kumpiga risasi marehemu jambo hilo tutalifanyia kazi baada ya
kukabilika kwa uchunguzi wao.
Maswali hayo hayakuweza
kuwaridhisha umati wa wananchi na upande wa familia ya marehemu na kumtaka kamanda
huyo awasiliane na mkuu wa wilaya ya Ulanga Francis Miti kwa kuhoji kwa nini
wewe Kamanda umetembea umabli mrefu kufika eneo la tukio na mkuu wako wa wilaya
ambaye yupo jirani ameshindwa kufika eneo la tukio ?.
Mzozo huo ulidumu kwa muda wa
masaa mawili bila kufikia muafaka katika siku ya pili baada ya tukio kutokea
ambayo kamanda wa polisi alishindwa kutimiza malengo yake, likiwemo
kuwashawishi ndugu wa marehemu wakubali kuutambua mwili wa marehemu, kupokea
uchunguzi wa daktari na kuchukua mwili wa marehemu jambo ambalo alilazimika
kuwasiliana na mkuu wa wilaya ili kufika eneo la tukio.
DC ULANGA.
Mkuu wa wilaya ya Ulanga
Francis Miti aliwasili katika eneo la tukio la mjira ya saa 10:30 alasiri na
kuanza kuwapa pole umati uliokuwa ukimsubiri ili kutatua kero za wananchi hao.
Miti baada ya kutoa pole kwa
wafiwa alianza kutoa ufafanuzi juu ya zana iliyojengeka kwa wananchi hao kuwa
marehemu amepigwa risasi katika zoezi la operesheni na kuwa askari hao hawakuwa
katika operesheni bali walikuwa katika zoezi la udhibiti na ufuatiliaji wa
mifugo katika bonde la hifadhi mto wa Kilombero na kuwa wanaobainika hukamatwa
na kutozwa faini kisha kuwapa ovyo waliende tena katika bonde la mto Kilombero.
“tukio hili hakuna
anayefurahia hata kidogo niwaeleze kuwa operesheni haipo kilichopo sasa ni udhibiti
na ufuatiliaji wa mifugo katika bonde la hifadhi mto wa Kilombero na operesheni
tayari ilishaisha tangu januari mosi mwaka huu” alisema Miti.
Hata hivyo mkuu huyo wa
wilaya naye alikumbana na maswali juu ya watendaji wake waliokuwa katika
operesheni na udhibiti na ufuatiliaji wa mifugo katika bonde la hifadhi mto
Kilombero na kuwa daktari wa mifugo wilaya Ulanga, Fredrick Sagamiko amekuwa
akidaiwa kukiuka utaratibu wa faini.
Mselengeti Mipawa (41)
alimweleza mkuu wa wilaya katika tukio hilo kuwa daktari huyo amekuwa akitoza
faini kati ya sh60,000 hadi 100,000 pindi anapokamata mifugo badala ya faini
iliyoidhinishwa na serikali ya kiasi cha sh44,000 kwa ng’ombe mmoja jambo
ambali wamekuwa wakilipia na kuwarudisha nyumba katika harakati za maendeleo.
Mipawa alimweleza mkuu huyo
wa wilaya kuwa daktari huyo wa mifugo wilaya ya Ulanga, licha ya kukiuka
utozaji wa faini pia amekuwa akimakata na mifugo ambayo haiku kwenye listi ya
ukamataji wa operesheni hiyo wakiwemo kukamata mifugo wakiwemo kondoo, mbuzi na
punda na kutozwa faini kubwa kuanzia kiasi cha sh 700,000 na kuendelea
kulinagana na uwingi wa mifugo hiyo.
Miti alisema kuwa baada ya
kupata tuhuma zinazo mwelekeza daktari wa mifugo wilaya Ulanga, Fredrick
Sagamiko yeye atawasilisha tuhuma hizo kwa mwajili wake ambaye ni mkurugezi wa
halmashauri ya wilaya ya Ulanga ili uchunguzi ufanyike na kama itabainika
sheria itafuata mkondo wake.
Aliwaeleza umati huyo kwa
kuwataka wafugaji waache tabia ya kuwashambulia askari na kuwataka askari nayo
kutotumia nguvu kubwa wakati wa vurugu pindi inapotokea hiyo itasaidia
kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya jeshi la polisi na wananchi.
Mkuu huyo alilazimika
kuwashawishi ndugu wa marehemu wakubaliane na ombi lao la kutaka wakatambue
mwili wa marehemu na kupokea uchunguzi wa daktari kisha kuchukua mwili wa
marehemu kwa ajili ya mazishi jambo ambalo lilishindikana kukubali ombi hilo
kutokana na kutotimiza madai yao.
Baada ya Kamanda wa polisi na
mkuu wa wilaya Ulanga kushindwa kuwashawishi ndugu wa marehemu kuchukua mwili
wa ndugu yao msafara wao uliondoka eneo hilo majira ya saa 12:30 jioni na siku
ya pili ya januari 28 mwaka huu ikifuatiwa na kutokubaliana hadi gazeti hili
liondoka katika eneo la tukio.
Awali Baba wa marehemu Katambi
Jidiga alisema kuwa marehemu alitokea mkoani Songea kuuza baadhi ya ng’ombe kwa
ajili kulipa madeni ya mifugo iliyokamatwa katika operationi, awali imetajwa
mbuzi 100 alilipa lakini saba, ngombe inadaiwa akikuwa akidaiwa 10 milioni na
mara ya tatu ngombe wake waliokamatwa na askari hao alikuwa akidaiwa sh milioni
3.
0 comments:
Post a Comment