BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KESI YA MWANGOSI YAPIGWA DANADANA, YADAIWA UPELELEZI BADO HAUJAKAMILIKA.

KWA UFUPI
Akizungumza na Mwananchi nje ya mahakama, Wakili wa Serikali,  Aldof  Maganda alisema kesi hiyo imeairishwa kwa kuwa upelelezi haujakamilika lakini pia ni kutokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutokuwepo mahakamani hapo.
KESI ya mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Channel  Ten mkoani  Iringa, Daudi Mwangosi imeahirishwa tena katika mahakama ya hakimu Mkazi kwa kile kinachoelezwa kuwa upelelezi haujakamilika na hakimu anayeendesha kesi hiyo kutokuwepo mahakamani hapo.
Kesi hiyo ya mauaji  inayomkabili  askari,   Pacificus Clephase mwenye namba G2372  imeahirishwa jana  mbele ya Hakimu, Mary Senapel  baada ya hakimu  anayesimamia kesi hiyo, Daines Lyimo kutokuwapo mahakamani  hapo pamoja na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.
Akizungumza na Mwananchi nje ya mahakama, Wakili wa Serikali,  Aldof  Maganda alisema kesi hiyo imeairishwa kwa kuwa upelelezi haujakamilika lakini pia ni kutokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutokuwepo mahakamani hapo.
Maganda alisema, kutokuwepo kwa hakimu anayesimamia kesi hiyo haina maana kuwa mtuhumiwa hatofikishwa mahakamani  bali kesi  hiyo huarishwa na kupangiwa tarehe nyingine.
Kesi  hiyo iliyofunguliwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya askari huyo, imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo  mtuhumiwa kuugua, Serikali kukosa mafuta ya gari  ya kumfikisha mtuhumiwa  mahakamani  na jana ya hakimu kutokufika  mahakamani.
Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo alipokuwa akiwajibika katika kazi zake za kutafuta habari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kufanya mikutano ya ndani ya kuimarisha chama.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: