Kwa ufupi
“Hiki ni kiwango cha juu kabisa kwa nchi kuweza
kukopa kutoka kwenye masoko ya kimataifa, deni limeongezeka kwa dola
456.1 milioni katika kipindi cha mwaka mmoja tu tangu Oktoba 2011,”
alisema Mwakagenda.Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia ya Tanzania Coalition on Debt and
Develompent (TCDD), Hebron Mwakagenda akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana, kuhusu kuongezeka kwa deni la taifa kufikia
kiasi cha Sh22 trilioni hadi Oktoba mwaka jana. Kulia ni Ofisa Mipango,
Boniface Komba. Picha na Fidelis Felix.
TAASISI isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na masuala ya
Madeni ya Taifa na Maendeleo (TCDD), imesema kitendo cha Serikali kukopa
fedha kwa ajili ya matumizi yasiyo na umuhimu pamoja na kuwalipa
watumishi wake mishahara, kimesababisha taifa kuwa na deni la Sh22
trilioni.
Imesema hali hiyo ni hatari hasa ikizingatiwa kuwa
miaka kadhaa iliyopita, Tanzania kupitia Mpango wa Nchi Maskini zenye
Madeni Makubwa (HIPC), ilifutiwa kiasi kikubwa cha madeni , lakini sasa
imeanza kukopa tena.
Taasisi hiyo pia imesema kitendo hicho kimechangia kuporomoka kwa uchumi wa taifa kwa sababu mikopo hiyo ina riba kubwa.
Imeeleza kuwa Serikali inakopa fedha hizo Benki Kuu (BoT), Benki za Biashara, Kampuni za Bima na Mashirika ya Hifadhi za Jamii, Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) na Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo ambayo kazi yake kubwa
ni kuishauri Serikali katika suala zima la deni la taifa na maendeleo,
Hebron Mwakagenda, alisema hadi kufikia Oktoba mwaka jana, deni la nje
lilikuwa Sh15.9 trilioni.
“Hiki ni kiwango cha juu kabisa kwa nchi kuweza
kukopa kutoka kwenye masoko ya kimataifa, deni limeongezeka kwa dola
456.1 milioni katika kipindi cha mwaka mmoja tu tangu Oktoba 2011,”
alisema Mwakagenda.
Alisema taarifa za Benki Kuu ya Tanzania
zinaonyesha kuwa deni la ndani limefikia Sh5.1 trilioni hadi kufikia
Oktoba mwaka jana na kwamba kiasi hicho ni sawa na ongezeko la Sh513
bilioni tangu mwaka 2011.
“Deni la ndani linakua kwa kasi kubwa inayotokana
na Serikali kuanza kukopa kwenye benki za biashara ambazo zinatoza riba
kubwa. Hii ni hatari kwa uchumi wa nchi,” alisema Mwakagenda.
Alisema zipo fedha zinazotumika kujenga barabara,
madaraja, majengo mbalimbali ya shule na vyuo, lakini kinachotakiwa ni
Serikali kufikiri mara mbili kabla ya kuamua kukopa na kuzitumia fedha
hizo za mkopo.Katika mapendekezo yao, Mwakagenda alisema wameitaka
Serikali kuwa na nidhamu katika kukopa kwa kuwa deni hilo limevuka
kiwango cha kimataifa.
“Pia umefikia wakati kwa Serikali kutokopa mpaka
ipate ridhaa ya Bunge kwa kuwa mikopo mingine haina faida kwa taifa
zaidi ya kuwaumiza wananchi,” alisema.
Alisema kuwa hadi sasa hakuna juhudi zinazofanywa na Serikali kuhakikisha kuwa inapata mikopo yenye riba nafuu.
Alisema kuwa hadi sasa hakuna juhudi zinazofanywa na Serikali kuhakikisha kuwa inapata mikopo yenye riba nafuu.
Alisema kitendo cha Serikali kuendelea kukopa
kutaifanya nchi kutoaminika tena na hivyo kutokopesheka iwapo kutaibuka
mahitaji ya lazima.
“Pia wawekezaji wanaweza kupunguza imani na
mazingira ya kiuchumi ya Tanzania na hivyo kutokuja kuwekeza, nchi
itashindwa kulipa madeni, thamani ya shilingi itashuka,” alisema
Mwakagenda.
Alisema Serikali inatakiwa kujifunza kwa nchi za
Hispania, Ugiriki na Ireland ambazo zimekubwa na matatizo ya kiuchumi
kutokana na kuwa na madeni makubwa.
“Tunaelezwa kwamba deni la taifa ni endelevu na bado nchi inakopesheka, sijui wanatumia takwimu za wapi,” alisema.
“Tunaelezwa kwamba deni la taifa ni endelevu na bado nchi inakopesheka, sijui wanatumia takwimu za wapi,” alisema.
0 comments:
Post a Comment