Mwanahabari wa RFI Kiswahili na
Bonesha FM nchini Burundi, Hassan Ruvakuki.
AFP PHOTO/Esdras Ndikumana.
MAHAKAMA kuu ya Gitega nchini Burundi, leo
imetoa hukumu ya kifungo cha miaka mitatu dhidi ya
Mwanahabari wa Radio Bonesha FM na Ripota wa RFIKiswahili Bw Hassan Ruvakuki.
Chama cha Waandishi wa Habari nchini Burundi UBJ kimelaani vikali hukumu hiyo kikisema kuwa Hassan Ruvakuki hana hatia na hastahili kifungo hicho.
Wakati Rufaa hiyo inaendelea mwaka jana, Mwendesha mashtaka wa Serikali alisema kuwal, Hassan Ruvakuki alikwenda nchini Tanzania jirani na mpaka wa Burundi ambapo alikutana na Waasi na kufanya Mahojiano nao na kusema kuwa hicho ni kitendo cha uhaini.
Hassan Ruvakuki na Mawakili wake walibainisha mahakamani kuwa alikwenda kufanya mahojiano na waasi ikiwa ni sehemu ya kazi za kawaida kwa Mwanahabari.
Baadhi ya Raia waliozungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio France International wameeleza juu ya matumaini yao kuwa Hassan Ruvakuki ataachwa huru kufuatia mbinyo uliotolewa na Wafadhili wa nje wa Burundi Mwaka jana.
Hassan Ruvakuki na wenzake walikamatwa na kufungwa mwishoni mwa mwaka 2011, na mara zote mahakamani kumekuwa na mvutano ambapo mwendesha mashtaka wa serikali alishindwa kuthitisha Mashtaka kwa Vielelezo.
0 comments:
Post a Comment