MARAIS wa Sudan na Sudan kusini wamekubaliana jana Jumamosi
(05.01.2013)kuhusu muda utakaopangwa kwa ajili ya utekelezaji wa masuala
muhimu,wakati walipokutana kwa faragha katika mji mkuu wa Ethiopia
,Addis Ababa.
Pande hizo mbili zimekubaliana kuwa makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano uliofanyika katika mwezi wa septemba mwaka jana yanapaswa kutekelezwa, bila masharti yoyote, amesema mpatanishi wa umoja wa Afrika , rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki.
"Jopo letu linatayarisha utaratibu wa utekelezaji wa makubaliano yote yaliyokwisha fikiwa kwa kupanga muda maalum, amesema Mbeki.
Rais wa Sudan kusini katika mazungumzo na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na mpatanishi Tambo Mbeki
Muda utakaopangwa utakamilika ifikapo Januari 13, Mbeki amesema. " Mkutano huo unapaswa kuhakikisha kuwa maamuzi muhimu yanachukuliwa ili kuunda eneo salama ambalo halitakuwa na shughuli za kijeshi," kama ilivyoelezwa katika mkutano wa Septemba.
Makubaliano ya awali
Pande zinazohusika zilikubaliana kuweka maeneo hayo katika mpaka wao wenye urefu wa kilometa 2,000 ambalo limekubalika.
Hakuna makubaliano ambayo yamefikiwa kuhusiana na mpaka wa karibu kilometa 500, na pia katika jimbo la Abyei ambalo linadaiwa na kila upande kuwa ni lake.
Rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki.
Eneo hilo lilikaliwa kwa muda na majeshi ya Sudan kusini mwezi wa Mei, baada ya jeshi la upande wa Sudan ya kaskazini kuondoka kufuatia kulikalia jimbo hilo kwa muda wa mwaka mmoja.
Kamishna wa jimbo la Abyei, Rahma Abdel-Rahman al-Nour, ameliambia shirika la habari la dpa kuwa suala la Abyei linaweza tu kutatuliwa mara masuala ya kiusalama yatakapokubaliwa.
Ramani inayoonesha jimbo la Abyei.
Katika hatua nyingine , muungano wa vyama vya upinzani pamoja na makundi ya vyama vya kijamii umetia saini makubaliano siku ya Jumamosi (05.01.2013) mjini Khartoum ukitoa wito wa kuangushwa kwa utawala wa Sudan na kufanya uchaguzi huru na wa haki.
Makubaliano hayo , yaliyopewa jina la "Mapambazuko mapya, " yanalenga katika kuleta suluhisho kwa uchumi wa Sudan pamoja na mzozo wa kisiasa , elimu na afya.
0 comments:
Post a Comment