Mstahiki meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa kushoto
akizoa taka huku Mkuu wa wilaya ya Ilala, RayMond Mushi kulia akimkusanyia
katika zoezi la kusafisha Kata ya Kivukoni lililoendeshwa na Kampuni ya Green
west pro yenye tenda ya kuzoa taka katika kata za mchafukoge,Kisutu na
Kivukoni.
Wakazi wa Kata ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam, wakiwa
wamejitokeza kwenye zoezi la kusafisha Manispaa ya Ilala liloendeshwa na
kampuni ya kuzoa taka Green West Pro katika kata tatu za Kivukoni ,mchafukoge
na Kisutu.
Mkuu wa wilaya ya Ilala kushoto, RayMond Mushi akizungumza na
wakazi wa kata ya Kivukoni waliojitokeza katika fukwe ya bahari ya Hindi
kufanya usafi ,baada ya mkandarasi wa kuzoa taka Green West Pro kufanya
uzinduzi huo,kulia ni Meya wa Manspaa ya Ilala Jery Silaa naye alishiriki kuzoa
taka.
Shughuli hiyo iliandaliwa na TANZANIA
News Forums ambalo ni jukwaa la habari kupitia shirika lake la Tanpress linalojihusisha na kazi
ya kukusanya habari kuzisambaza kwenye vyombo mbalimbali vya habari.
0 comments:
Post a Comment