Meneja wa blog jumamtanda, Juma Mtanda akiwa amepozi kwa picha katika mawe yaliyopo katika bustani ya Rock (ROCK GARDEN) ambako kwa sasa kutokana na ukame ulioukumba baadhi ya maeneo ya mkoa wa Morogoro umesababisha mto Morogoro kushindwa kutiririsha maji mengi kama ilivyokuwa miaka ya nyumba huku chanzo kingine kikidaiwa baadhi ya wananchi kulima kando na vyanzo vya maji na kusababisha hali hiyo.
Hapa ndipo panaonekana kuwa na maji mengi kuliko sehemu yo yote ndani ya bustani hiyo ambayo imetengenezwa katikati ya mto Morogoro.
Maji yakiwa yametuwama katika mawe baada ya kushindwa kutiririka kutokana na ukame huo.
Moja ya sehemu nyingine ya mto huo ikionekana ikiwa na maji kidogo.
Hapa ni sehemu za mto Morogoro zilizopita katikati ya bustani ya Rock ikiwa inaonekana mawe tupu ambapo kipindi cha masika kumekuwa kukitiririsha maji mengi yenye uwezo wa kumsomba binadamu ambapo eneo hilo limekuwa likitumiwa na watu wa rika mbalimbali kwa ajili ya mapumziko ikiwemo na kuongea.
0 comments:
Post a Comment