Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Manispaa ya Morogoro Roman Luoga
akimfundisha namna ya kuandika namba kwa mwanafunzi wa darasa la kwanza
katika shule hiyo, Joyce Telephory (7) huku wenzake Lydia Peter (7)
katikati na Joshuoa Mbote wa kwanza kushoto nao wakifuatilia jambo
wakati wa somo la hisabati kwa wanafunzi wa darasa la kwanza waliojiunga
na elimu ya msingi katika shule hiyo mkoani hapa.
Hapa Mwalimu mkuu huyo akifundisha somo la hesabati, haya semeni wote kwa kuhesabu moja, mbili, tatu, Sawa, je lake sawa na ngapi ? jibuni wote kwa pamoja wamanafunzi, wanaitikia kwa sauti kubwaaa.....tatu mwalimu !!! kazi ndiyo imeanza.
Wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Bungo Manispaa ya Morogoro wakimsikiliza mwalimu mkuu wa shule hiyo Roman Luoga
(hayupo pichani) wakati akiwafundisha namna ya kuandika namba wakati wa somo la hisabati ikiwa ni siku ya kwanza baada ya shule kufunguliwa Jan 07/ 2013.
SIJUI UGALI NITAUWAHI NYUMBANI ???.
Mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Bungo Manispaa hiyo Mikidadi Mtanda akielekea stendi kuu ya daladala wakati akirejea nyumbani baada ya kumaliza masomo ya kutwa baada ya kufunguliwa kwa muhula wa masomo kwa mwaka 2013.
HEKA HEKA ZA KUWARUDISHA WANAFUNZI NYUMBANI.
HEKA HEKA ZA KUWARUDISHA WANAFUNZI NYUMBANI.
Hii ni hatari kwa afya ya mtoto kutokana na kuvaa nguo nyepesi ambayo upepo hupenda moja kwa moja hadi mwilini jambo ambalo husababisha kifua huku mwendesha pikipiki naye akiwa hana kofia ngumu (Elment) ni uvunjaji wa sheria wa usalama barabara.
Hii ndiyo kikosi cha usalama barabara upakiaji wa namna hii huiita mishikaki jambo ambalo wanalipiga vita kutokana na wahusika kushindwa kujali usalama wao pamoja na abiria.
Huyu naye ni miongoni mwa waendesha baiskeli ambaye amevunja sheria za usalama barabarani kwani sheria inamtaka kuvaa kofia ngumu na kupakia abiria mmoja, hapa anaonekana akiwarejesha nyumba mwaanafunzi na mungine ambaye hakuweza kufahamika licha ya kufikia umri wa kwenda shule.
Mzazi akiwa na watoto wake akichagua sare za shule wakati wa maandalizi ya ufunguzi wa muhula wa masomo kwa mwaka 2013.
Hapa mzazi akimjaribisha mwanao sare wakati akiwa katika mchaakato wa kununua katika mnada wa Sabasaba unaofanyika kila jumapili katika Manispaa ya Morogoro.
Hapa wanafunzi wa shule za sekondari wakichagua viatu kwa jili ya maandalizi ya shule mara baada ya kufunguliwa.
Wazazi wakinunua vifaa ya shule katika mnada wa soko la SabaSaba mjini hapa.
0 comments:
Post a Comment