POLISI MMOJA ATOROKA ENEO LA TUKIO NA BUNDUKI YAKE.
IGP SAIDI MWEMA.
WANANCHI wilayani Karagwe, Mkoa wa Kagera, wamewaua polisi wawili wa Kituo cha
Polisi Benako, kilichoko Wilaya ya Ngara. Polisi hao waliuawa kwa silaha za
jadi, baada ya kudhaniwa kuwa ni majambazi waliokuwa na meno ya tembo.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi katika Kijiji cha Kasheshe, Kata ya
Rugu, wilayani Karagwe, baada ya askari hao kudaiwa kujihusisha na wizi wa meno
ya Tembo yenye uzito wa kilogramu 34.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kagera,
Philipo Kalangi, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5:30 usiku, ambapo
askari wawili waliuawa na wananchi baada ya kukutwa na meno ya Tembo kwenye
gari aina ya Noah, ambalo namba zake za usajili hazikujulikana.
Gari hilo lililokuwa na mzigo huo, nalo liliteketezwa kwa moto na wananchi hao.
Kamanda Kalangi aliwataja askari hao waliouawa kuwa ni wenye namba E 1446
Sajenti Thomas Magiro na E 8889 Koplo Damasi Kisheke, wote kutoka kituo cha
Polisi Benako, Ngara.
Pamoja na vifo hivyo, alisema askari mwingine ambaye jina lake halijajulikana,
alifanikiwa kutoroka na kupotelea kusikojulikana akiwa na silaha. Jeshi la
Polisi linaendelea kumsaka ili akajibu tuhuma zinazomkabili.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Kalangi, alisema awali askari hao walikuwa
wakitokea katika Kijiji cha Kasheshe wakiwa wamepakia meno ya Tembo.
“Walipokuwa njiani wananchi wa kijiji hicho, walitoa taarifa kwa wananchi
wengine na kufunga barabara kwa mawe kisha gari la watuhumiwa lilipofika hapo,
watuhumiwa walihojiwa na wananchi na kuonyesha vitambulisho vyao, lakini
wananchi hawakutaka kuwaelewa.
“Wananchi baadaye waliwashambulia watuhumiwa hao na kisha gari walilokuwanalo
waliliteketeza kwa moto, jambo lililopelekea askari wawili kupoteza maisha na
mmoja alifanikiwa kutoroka akiwa na silaha,” alisema Kamanda Kalangi.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Nyakahanga iliyoko Wilaya ya Karagwe, Dk.
Andrew Cesari, alithibitisha kupokea miili ya marehemu hao.
Alisema uchunguzi wa kitabibu umeonyesha askari hao walifariki baada ya kipigo
kikali kilichosababisha majeraha na kuvuja damu nyingi.
Wakati hao wakisema hayo, chanzo chetu kingine cha habari kutoka Karagwe
kilisema askari hao walikuwa wanatoka katika Kijiji cha Nyakakika Bushangaro,
kilichopo Tarafa ya Nyabiyoza wilayani Karagwe.
Chanzo hicho kilisema kuwa, askari hao kutoka Ngara, walikwenda Karagwe
kuchukua meno ya Tembo kwa mwananchi mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Kayengo.
Chanzo hicho kilisema kuwa, askari hao walikuwa na uhusiano wa kibiashara na
Kayengo na kwamba walikwenda kwake kuuziana meno hayo kwa kuwa wana mahusiano
ya muda mrefu kibiashara.
“Baada ya askari hao kufika kwa mwenzao huyo, inaonekana walishindana kwani
baadaye walimgeuzia kibao na kuamua kuchukua meno hayo bila kumlipa mhusika.
“Inavyoonekana Kayengo hakufurahishwa na kitendo hicho na ndipo alipoamua
kupiga simu kwa jamaa zake walioko Kijiji cha Kasheshe, kwamba kuna majambazi
wamemvamia na kuchukua mali zake na kuondokana nazo wakielekea Kasheshe.
“Taarifa hizo ziliwahamasisha wananchi, kwa hiyo, walikusanyana na kuweka
kizuizi barabarani ili majambazi hao wakifika waweze kudhibitiwa.
“Sasa basi, askari hao walipofika kijijini hapo wakiwa na mali kwenye gari,
walikumbana na kizuizi hicho na walijitahidi kupiga risasi hewani ili
kusambaratisha umati wa wananchi lakini walizidiwa nguvu kutokana na wingi wa
wananchi.
“Kwa maana hiyo, polisi walianza kushambuliwa kwa silaha za jadi na mwishowe
wawili wakapoteza maisha na mmoja akafanikiwa kutoroka na kukimbia hadi Kituo
Kidogo cha Polisi cha Nyakasimbi kilichopo kijijini hapo.
“Ila baadaye tumepata taarifa, kwamba askari huyo alifikishwa katika Kituo cha
Polisi cha Wilaya ya Karagwe cha Nyakahanga,” kilisema chanzo chetu hicho.
Kuuawa kwa askari hao ni mwendelezo wa mauaji dhidi ya polisi, kwani wiki mbili
zilizopita askari wawili wilayani Ngara waliuawa na wananchi baada ya kudaiwa
kumuua fundi pikipiki.
CHANZO http://www.mtanzania.co.tz
WANANCHI wilayani Karagwe, Mkoa wa Kagera, wamewaua polisi wawili wa Kituo cha Polisi Benako, kilichoko Wilaya ya Ngara. Polisi hao waliuawa kwa silaha za jadi, baada ya kudhaniwa kuwa ni majambazi waliokuwa na meno ya tembo.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi katika Kijiji cha Kasheshe, Kata ya Rugu, wilayani Karagwe, baada ya askari hao kudaiwa kujihusisha na wizi wa meno ya Tembo yenye uzito wa kilogramu 34.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kagera, Philipo Kalangi, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5:30 usiku, ambapo askari wawili waliuawa na wananchi baada ya kukutwa na meno ya Tembo kwenye gari aina ya Noah, ambalo namba zake za usajili hazikujulikana.
Gari hilo lililokuwa na mzigo huo, nalo liliteketezwa kwa moto na wananchi hao.
Kamanda Kalangi aliwataja askari hao waliouawa kuwa ni wenye namba E 1446 Sajenti Thomas Magiro na E 8889 Koplo Damasi Kisheke, wote kutoka kituo cha Polisi Benako, Ngara.
Pamoja na vifo hivyo, alisema askari mwingine ambaye jina lake halijajulikana, alifanikiwa kutoroka na kupotelea kusikojulikana akiwa na silaha. Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka ili akajibu tuhuma zinazomkabili.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Kalangi, alisema awali askari hao walikuwa wakitokea katika Kijiji cha Kasheshe wakiwa wamepakia meno ya Tembo.
“Walipokuwa njiani wananchi wa kijiji hicho, walitoa taarifa kwa wananchi wengine na kufunga barabara kwa mawe kisha gari la watuhumiwa lilipofika hapo, watuhumiwa walihojiwa na wananchi na kuonyesha vitambulisho vyao, lakini wananchi hawakutaka kuwaelewa.
“Wananchi baadaye waliwashambulia watuhumiwa hao na kisha gari walilokuwanalo waliliteketeza kwa moto, jambo lililopelekea askari wawili kupoteza maisha na mmoja alifanikiwa kutoroka akiwa na silaha,” alisema Kamanda Kalangi.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Nyakahanga iliyoko Wilaya ya Karagwe, Dk. Andrew Cesari, alithibitisha kupokea miili ya marehemu hao.
Alisema uchunguzi wa kitabibu umeonyesha askari hao walifariki baada ya kipigo kikali kilichosababisha majeraha na kuvuja damu nyingi.
Wakati hao wakisema hayo, chanzo chetu kingine cha habari kutoka Karagwe kilisema askari hao walikuwa wanatoka katika Kijiji cha Nyakakika Bushangaro, kilichopo Tarafa ya Nyabiyoza wilayani Karagwe.
Chanzo hicho kilisema kuwa, askari hao kutoka Ngara, walikwenda Karagwe kuchukua meno ya Tembo kwa mwananchi mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Kayengo.
Chanzo hicho kilisema kuwa, askari hao walikuwa na uhusiano wa kibiashara na Kayengo na kwamba walikwenda kwake kuuziana meno hayo kwa kuwa wana mahusiano ya muda mrefu kibiashara.
“Baada ya askari hao kufika kwa mwenzao huyo, inaonekana walishindana kwani baadaye walimgeuzia kibao na kuamua kuchukua meno hayo bila kumlipa mhusika.
“Inavyoonekana Kayengo hakufurahishwa na kitendo hicho na ndipo alipoamua kupiga simu kwa jamaa zake walioko Kijiji cha Kasheshe, kwamba kuna majambazi wamemvamia na kuchukua mali zake na kuondokana nazo wakielekea Kasheshe.
“Taarifa hizo ziliwahamasisha wananchi, kwa hiyo, walikusanyana na kuweka kizuizi barabarani ili majambazi hao wakifika waweze kudhibitiwa.
“Sasa basi, askari hao walipofika kijijini hapo wakiwa na mali kwenye gari, walikumbana na kizuizi hicho na walijitahidi kupiga risasi hewani ili kusambaratisha umati wa wananchi lakini walizidiwa nguvu kutokana na wingi wa wananchi.
“Kwa maana hiyo, polisi walianza kushambuliwa kwa silaha za jadi na mwishowe wawili wakapoteza maisha na mmoja akafanikiwa kutoroka na kukimbia hadi Kituo Kidogo cha Polisi cha Nyakasimbi kilichopo kijijini hapo.
“Ila baadaye tumepata taarifa, kwamba askari huyo alifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Karagwe cha Nyakahanga,” kilisema chanzo chetu hicho.
Kuuawa kwa askari hao ni mwendelezo wa mauaji dhidi ya polisi, kwani wiki mbili zilizopita askari wawili wilayani Ngara waliuawa na wananchi baada ya kudaiwa kumuua fundi pikipiki.
1 comments:
Hayo ndiyo madhara ya kuwafumbia macho wahamiaji haramu. Wanaleta spirit na mbegu mbaya za kwao wanakotoka. Tukio la Mugoma Ngara lina mbegu mbaya ya Warundi wakorofi ndiyo maana baada ya mauaji karibu wahusika wengi walivuka mpaka wakakimbilia Burundi.Na wiki 3 baadaye tunasikia hili la Karagwe na huko ni kazi ya mbegu mbaya ya Wanyarwanda. Tena hawa ni wabaya zaidi maana wamekuja Karagwe/Ngara na ming'ombe kibao, wana haribu mazao ya wazawa/wanavijiji wetu na serikali inawaangalia tu.Tukiendelea kubweteka miaka 3 -5 ijayo YATATOKEA MAKUBWA ZAIDI KAGERA.
Post a Comment