DR Shein akihutubia wana CCM katika Kusheherekea miaka
36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shain amewatoa mashaka WATU wanaohoji kutokuwepo
kwa hati halisi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema hati hiyo ipo
na iwapo hawaamini wanaweza kwenda Umoja wa Mataifa New York.
Amesema Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar chimbuko la kuasisiwa kwake kulitokana na ridhaa ya wananchi wa pande
mbili za Muungano na kuwataka wanaowababisha wananchi kwa maneno ya mitaani
kuacha kufanya hivyo kwa sababu kila swali lao lina jawabu lake.
Dk Shein ambaye pia ni Makamo
Mwenyeki wa CCM Zanzibar amesema kuundwa kwa Muungano halikuwa ni jambo la
kubahatisha bali lina malengo yaliokusudiwa kabla ya kupatikana Uhuru ya
Tanganyika mwaka 1961 na kufanyika kwa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar Januri
12,1964.
Amesema wenye wasiwasi na kutokuwepo
kwa hati ya Muungano wamfuate ikulu awaonyeshe chumba walichokutana Mwalimu
Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume na kufanya makubaliano ya mwisho kabla ya
kuunganisha nchi zao.
Ameeleza kuwa madhumuni ya vyama vya
TANU na ASP yalilingana tokea vyama hivyo vikiwa katika harakati zake za
kujikomboa hivyo kurahisisha hata kazi ya kuziunganisha nchi hizo mwaka 1964
pia vyama hivyo na kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977.
Aidha Makamo huyo Mwenyekiti wa CCM
amewaeleza wananchi kuwa Mapinduzi ya Zanzibar ndiyo Uhuru kamili wa visiwa vya
Unguja na Pemba huku akiwataka wananchi kutowasiliza watu wanaopotosha ukweli
na kuwataka kuacha kufanya hivyo.
Dk Shein amesema watu wanaobeza
ukweli huo hawana nguvu ya hoja bali wana lengo la kuwagawa wananchi ili waweze
kuyafikia matarajio yao ambayo amesisitiza yanapaswa kupuuzwa na kila mpenda
amani na umoja.
Amewataka watu hao kupuuzwa
kwasababu hawajui wafanyalo na kwamba wanamangamanga ili kutaka kuwagawa
wananchi bila ya kufikiri kwa makini .
Akizungumzia faida za Muungano Dk
Shein amesema kiuhalisia wananchi wa Zanzibar ndiyo wanaofaidika na Muungano
huo kwani kila uendepa katika Tamnzania Bara kuna wazanaziabri waliotamalaki na
kuwekeza miradi na mitaji .
Alisema Zanzibar inafaidika na siko
la Bara ambapo kabla ya Mapinduzi ilikuwa ikiagiza bidhaa za vyakula na
mahitaji mengine kutoka nchi za Pakistan, Japan na mashariki ya mbali jambo
ambalo sasa linapatikana kutoka Mikoa ya Bara.
Kwa upnde wake Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizunguimza kabla ya kumkaribisha Dk Shein ,amesema
nguvu ya umoja na maelewano kati ya visiwa vya Unguja na Pemba inatokana na
kuwepo kwa Muungano na kusema nje ya jambo hilo lolote linaweza kutokea.
Vuai amesema Muungano wa Tanzania
licha ya kuleta tija za kiuchumi lakini pia kwa kipindi chote cha miaka 49 ya
kuwepo kwake umelinda na kusimamia usalama wa raia na mali zao.
Amesema hata pale Tanznia
ilipovamiwa na majeshi ya Idd Amini mwaka 1978,wanajeshi wa Zanzibar waliingia
vitani ili kuihami nchi yao vikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba na kwamba nje
ya Muungano umoja huo unaweza kuparaganyika .
Naibu huyo Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar,amesema CCM itaendelea kujivunia matunda ya TANU na ASP kutokana na
kupigania kwao maslahi ya watu waliokuwa wakikandamizwa na kubaguliwa katika
ardhi ya nchi zao.
Amesema vyama hivyo kwa pamoja
vilihakikiisha vinajenga misingi imara ya heshama na utu kwa kila binadamu na
kuondosha matabaka,ubaguzi wa rangi na maonevu hadi pale vilipoamua kuunganisha
nguvu zake na kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi mwaka 1977.
0 comments:
Post a Comment