******************
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameunga mkono hoja binafsi ya Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia kuhusu udhaifu wa elimu nchini akisema, kuna udhaifu mkubwa katika sekta hiyo.
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameunga mkono hoja binafsi ya Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia kuhusu udhaifu wa elimu nchini akisema, kuna udhaifu mkubwa katika sekta hiyo.
Lowassa
alisema hayo jana katika Mahafali ya 13 ya Kidato cha Sita ya Shule ya
Sekondari Benjamini William Mkapa, jijini Dar es Salaam ambapo alieleza
kuwa sekta ya elimu inahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuweza kuzalisha
wahitimu wenye tija kwa taifa.
”Kuna
tatizo la hali ya elimu nchini, tushirikiane wazazi, jamii, wanasiasa na
wataalamu, tuangalie jinsi ya kusaidia sekta ya elimu kwa maana
tutasaidia watoto wa nchi yetu,”alisema Lowassa.
Katika
mahafali hayo, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli mkoani Arusha
kupitia (CCM) aliwakabidhi vyeti jumla ya wahitimu 330, kati yao
wavulana 263 na wasichana 67 .
“Wabunge
wengi bungeni tunakubaliana kwamba ipo haja ya kutazama upya suala zima
la mitalaa ya elimu katika nchi yetu kwani elimu iliyopo inawaandaa
watafuta kazi na siyo wanaotaka kujiajiri,”alisema Lowassa.
Alisema
kuwa kukiwa na mfumo mzuri wa elimu wenye kuwaandaa wahitimu walio na
uwezo wa kujiajiri wenyewe na kutokutegemea kuajiriwa taifa litapiga
hatua.
Alihamisi
wiki hii, Mbatia aliwasilisha bungeni Hoja Binafsi kuhusu Udhaifu wa
Elimu Tanzania, akitaka mfumo mzima unaosimamia elimu nchini ufumuliwe,
hoja iliyogeuka ‘kaa la moto’ kwa Serikali.
Baada ya
majadiliano marefu kuhusu kuundwa kwa kamati ya kuchunguza mitalaa, sera
na mihutasari ya elimu, hoja mbalimbali zilitolewa, huku baadhi ya
wabunge wakitaka Kamati ya Bunge, wengine wakitaka iundwe tume huru ya
kufuatilia suala hilo.
Mjadala
huo uliendelea juzi asubuhi kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk
Shukuru Kawambwa kusimama na kutetea mfumo wa elimu uliopo na
kusisitiza kuwa Serikali inayo mitalaa, kabla ya wabunge kuchangia na
Mbatia kuhitimisha akitaka kuiondoa hoja yake hadi Serikali
itakapowasilisha mitalaa hiyo ya elimu bungeni.
Hata
hivyo, Naibu Spika, Job Ndugai alikataa pendekezo la Mbatia na kutumia
kanuni za Bunge za kuipitisha hoja hiyo kwa kuwahoji wabunge.
Baada ya
hoja hiyo kupitishwa kwa kuungwa mkono na wabunge wengi wa CCM, hali
hiyo iliwaudhi wabunge wa upinzani, ambao waliamua kutoka nje ya ukumbi.
Baadaye
walikubaliana kumshtaki Waziri Kawambwa kwenye Kamati ya Bunge ya
Mamlaka ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, wakimtaka ajiuzulu kwa
kulidanganya Bunge, ikishindikana watalipeleka suala hilo kwa mamlaka
zilizomteua. MWANANCHI
Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/2013/02/lowassa-amuunga-mkono-mbatia.html#ixzz2JoYRckAV
0 comments:
Post a Comment