Meli ya kivita ya kupambana na uharamia aina ya
Anti Submarine iitwayo Marshal
Shaposhnikov’, ilipokuwa ikiingia na kasha baadae kutia nanga katika
bandari ya Dar es Salaam, kwa ziara fupi yenye lengo la kuimarisha urafiki
baina ya Jeshi la Wanamaji wa Tanzania na Urusi.
Wakati nchi ya Somalia ikiendelea kuwa kitovu cha uharamia,
jumuiya ya kimataifa ilikubaliana kudhamiria kupambana na vitendo hivyo viovu.
Lakini hadi sasa, wakati nchi nyingine zikitumia mbinu mbalimbali katika
mapambano hayo, ni nchi za Russia, India na China pekee zinazosindikiza meli
zao za biashara na nyinginezo ili kuzilinda na uharamia.
Meli hiyo imewasili siku ya Jumamosi na inategemea kuondoka
kesho, Jumatano.
Balozi wa Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander
Rannikh akipokea salamu kutoka kwa kiongozi mkuu Rear Admiral Vladimir
Vdovenko wakati alipotembelea meli hiyo bandarini.
Balozi
Rannikh akiambatana na kiongozi wa wanajeshi waliofatana na meli hiyo Rear
Admiral Vdovenko
Kwa pamoja, Balozi Rannikh na wanajeshi wa Kirusi waliimba
wimbo wao wataifa wakiwa katika meli.
Balozi
Rannikh akiwapongeza wanajeshi wake kwa kufika Dar es Salaam, Tanzania na
kuwakaribisha nchi pia.
Baada
ya salamu hizo, Balozi Rannikh nae alikaribishwa keki na mmvinyo iliyoandaliwa
na wanajeshi katika meli.
Wanajeshi
wa Kirusi wakionesha umahili wao wa ukakamavu muda mfupi kabla Balozi wan chi
yao Mheshimiwa Rannikh hajapita mbele yao.
0 comments:
Post a Comment