BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NCHI YA TUNISIA YAKUMBWA TENA NA GHASIA, NI BAADA YA KUUAWA KWA KIONGOZI WA UPINZANIA CHOKRI BELAID.

Waandamanaji nchini Tunisia baada ya kuuawa kwa kiongozi wa upinzani Chokri Belaid, Februari 7,2013
 Waandamanaji nchini Tunisia baada ya kuuawa kwa kiongozi wa upinzani Chokri Belaid, Februari 7,2013.

Mkosoaji huyo mkubwa wa serikali alipigwa risasi kadhaa akitoka nyumbani kwake Jumatano.

Chama kikuu cha wafanyakazi huko Tunisia kimeitisha mgomo wa kitaifa Ijumaa, ili waungane na waombolezaji kwenye mazishi ya kiongozi wa upinzani  aliyeuawa Chokri Belaid .

Mgomo huo ulitangazwa  Alhamisi usiku na umoja wa vyama vya wafanyakazi wa Tunis, na kuzusha ghasia za kisiasa ambazo zilipelekea  chama tawala  cha kiislam kukataa mpango uliowekwa na waziri mkuu wake kuunda serikali mpya.Polisi wa kutuliza ghasia pia walipambana  na waandamanaji kwenye mji mkuu kwa siku ya pili.

Waziri mkuu Hamadi Jebali alitangaza  Jumatano usiku mpango wake wa kufuta  serikali ya sasa baada ya ghasia kulipuka  katika mji mkuu kufuatia kuuwawa kwa Belaid.

Alisema serikali mpya itajumwisha wataalam wasiokuwa na uhusiano wowote na vyama vya kisiasa. 

Tangazo hilo lilipokelewa kwa furaha kubwa na viongozi wa upinzani.

Watu wasiojulikana walimpiga risasi mara kadhaa mkosoaji huyo mkubwa wa serikali, alipokuwa akiondoka nyumbani kwake Jumatano. Kufikia sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na kifo chake.  
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: