Kwa ufupi
Zanzibar, nchi yenye wakazi zaidi ya milioni moja,
na wenye kufuata utamaduni wa Kiislamu ni miongoni mwa nchi zilizokuwa
na idadi kubwa ya wasichana wanaolazimishwa kuolewa wakiwa na umri mdogo.
INAKISIWA kuwa katika kila dakika moja, watoto wa kike 19 wenye umri chini ya miaka 18 wanaolewa kwa nguvu duniani.
INAKISIWA kuwa katika kila dakika moja, watoto wa kike 19 wenye umri chini ya miaka 18 wanaolewa kwa nguvu duniani.
Kuwa mtoto wa kike katika nchi zinazoendelea
katika Bara la Asia (asilimia 46) na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara
(asilimia 38) ni mbaya zaidi kutokana na kukithiri kwa ndoa za mapema na
za kulazimishwa.
Kwa mujibu wa shirika la kimaitaifa la kuchangia
maendeleo ya watoto (PLAN) wasichana zaidi ya millioni 14 wanaolewa
wakiwa na umri chini ya miaka 18 katika nchi za Kusini mwa Jangwa la
Sahara. Nchi za Chad, Niger, na Mali zinaongoza!.
Hata hivyo inawezekana kuwa Zanzibar, nchi yenye
wakazi zaidi ya milioni moja, na wenye kufuata utamaduni wa Kiislamu ni
miongoni mwa nchi zilizokuwa na idadi kubwa ya wasichana wanaolazimishwa
kuolewa wakiwa na umri mdogo.
Utafiti uliyofanywa na Chama cha Waandishi wa
Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) umeonesha kuwepo kwa tatizo la
kuwalazimisha wanafunzi kuolewa mapema visiwani Zanzibar, mjini na
vijijini, hata hivyo, ripoti ya utafiti huo umebaini kuwa takwimu
zilizopatikana ni chache kulinganisha na hali halisi kutokana na kuwa
ndoa nyingi za kulazimishwa hazifikishwi katika vyombo vya sheria.
Kwa jumla takwimu za Wizara ya Elimu, ni kesi 32
za kulazimishwa kuolewa zilirekodiwa mwaka 2011, na kwamba kesi nyingi
hazifikishwi polisi isipokuwa wanafamilia husuluhishana wenyewe kwa
wenyewe na kwa wale wanaokataa suluhu ndiyo wanaofikishana polisi na
mahakamani.
Baadhi ya watu waliohojiwa katika utafiti wa
TAMWA, walieleza kuwa ndoa za kulazimishwa zinaendelea kutokana na
kulazimishwa au mimba za utotoni kwa wanafunzi.
Baadhi ya mifano ya ndoa za kulazimishwa ni Wilaya
ya Micheweni, Pemba ambako kwa wastani wanafunzi kumi (10) hukatishwa
masomo na kuolewa katika skuli za Tumbe na Micheweni kila mwaka.
Wilaya ya Magharibi, Unguja- mwaka 2011 jumla ya
kesi 13 za wanafunzi kupata mimba zilipelekwa Wizara ya Elimu kwa
uchunguzi ambapo baadhi yao waliolewa.
Wilaya ya Kaskazini A, Unguja- tatizo la watoto wa
kike kukatishwa masomo na kuolewa lipo kwa kiasi kikubwa katika Wilaya
ya Kaskazini “A” Mkuu wa Wilaya, Riziki Juma Simai alisema tatizo hilo
lipo lakini hakuna anaekwenda kuripoti au kushtaki kwa sababu inapotokea
mwanafunzi kubeba mimba wazazi wanachukua uamuzi wa kumuoza.
“Iwapo wao viongozi wa wilaya wanapata taarifa
basi harusi zinavunjwa, ili mtoto wa kike aendelee na masomo, na hii
inakuja iwapo anayeolewa hana mimba na mwenyewe anataka kuendelea na
masomo,” anasema Simai.
Anaongeza:
“Tuna tatizo kwa sababu wazee wanachukua uamuzi wa kufanya harusi wenyewe na Serikali ikiingilia basi unaona harusi inafanywa haraka haraka lakini hata hivyo tunapopata habari tu tunachukua hatua za kuivunja hiyo harusi lakini wakati mwingine wazee wanakuwa na ukaidi sana”.
“Tuna tatizo kwa sababu wazee wanachukua uamuzi wa kufanya harusi wenyewe na Serikali ikiingilia basi unaona harusi inafanywa haraka haraka lakini hata hivyo tunapopata habari tu tunachukua hatua za kuivunja hiyo harusi lakini wakati mwingine wazee wanakuwa na ukaidi sana”.
0 comments:
Post a Comment