Mratibu wa taasisi ya Shikamana  Brittany Karima Cesarini( kulia ) akiwakabidhi vipeperushi   vyenye  ujumbe wa tuungane kutokomeza unyanyasaji  Mozes Festo wa shule ya sekondari ya Mbezi Beach  na Husna Methew wa shule ya sekondari ya Jitegemee, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutoa alimu ya kutokomeza unyanyasaji kwa wanafunzi wa shule  mbalimbali za sekondari jijini Dar es Salaam, ufunguzi huo ulifanyika  katika ukumbi wa Theater 1 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mratibu wa taasisi ya Shikamana  Brittany Karima Cesarini( kushoto ) akiwahutubia wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar es Salaam,  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutoa alimu ya kutokomeza unyanyasaji kwa wanafunzi wa shule  mbalimbali za sekondari jijini Dar es Salaam, ufunguzi huo ulifanyika  katika ukumbi wa Theater 1 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mhadhili wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Vicensia Shule ,Wakili wa kujitegemea Laetitia Petro  na  mjumbe wa Shikamana Ansia Albert
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam, wakiwa na vitabu  vilivyo andikwa Hali Halisi ya Kijinsia Nchini Tanzania wakati wa uzinduzi wa utoaji wa elimu kwa shule za sekondari juu ya  unyanyaaji wa kijinsia ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya utoaji wa mahusiano ya mazuri ya kimapenzi  kwa vijana .Shikamana  wamedhamilia kuleta mabadiliko juu ya utoaji wa elimu kwa jamii ili kupambana na aina zote za unyanyasaji  na udhalilishaji  wa kijinsia.