Sumaye aliyasema hayo jana mjini hapa, alipotembelea Taasisi ya
Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, iliyopo wilayani Arumeru, mkoani
Arusha.
“Kugundulika kwa rasilimali hakuifanyi nchi kuwa tajiri, bali rasilimali hizo zitakapoweza kugeuzwa na kuwa bidhaa hapo ndipo utajiri unaweza kuhesabiwa.
“Pamoja na uwepo wa rasilimali kama gesi iliyogundulika mkoani Mtwara, bado kuna haja ya kuwa na wataalamu wasomi watakaobadilisha rasilimali zilizopo kuwa bidhaa.
“Pia bila kuwa na mapinduzi ya viwanda, bado itakuwa vigumu kupiga hatua ya maendeleo pamoja na kuendelea kuwa na rasilimali zilizopo nchini.
“Kwa hiyo ni imani yangu kwamba, Taasisi ya Mandela itakuja na majibu ya rasilimali zinazotuzunguka nchini, ikiwamo hiyo gesi ambayo sasa kila mmoja anaizungumzia,” alisema Sumaye na kuongeza:
“Muda wowote mtakaonihitaji na mkiamini kwamba naweza kufanya jambo kwenye taasisi hii, nipo tayari kutoa msaada, nawakaribisha sana msisite kuniona,” alisema Sumaye.
Akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo, alikubali kuwa mwanachama wa mfuko utakaosaidia kutafuta fedha kwa ajili ya kusaidia mambo mbalimbali, ikiwamo tafiti zinazofanywa na zitakazofanywa na wanafunzi wa taasisi hiyo.
Katika hatua nyingine, Sumaye aliipongeza taasisi hiyo kwa kuanzisha mfumo wa kusoma vitabu kwa kutumia njia ya mtandao (TEHAMA).
Alisema kwamba, katika kuboresha mfumo huo kwa shule za msingi, ni vema taasisi hiyo ikaishirikisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ili nayo iweze kutoa mchango mpana wa kurahisisha mfumo huo.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo, Professa Burton Mwamila, akizungumzia mfumo huo, alisema zinahitajika zaidi ya Sh milioni 21 kwa ajili ya kuanza kutumika.
“Tumeweza kuanza na Shule ya Msingi Nganana kwa kuwasaidia kupata au kusoma vitabu vingi kwa kutumia TEHAMA, kwa sababu shule hii ipo jirani na taasisi yetu,” alisema Prof. Mwamila.
“Shule ya Nganana ina wafunzi 400 na wanafunzi 100 walio darasa la nne na darasa la saba ndio wanaohitaji kutumia mfumo huu wakati wa kusoma vitabu,” alisema Profesa Mwamila.

0 comments:
Post a Comment