BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA YA MCHEZO WA LIGI KUU VODACOM POLISI NA AFRICAN LYON UWANJA WA JAMHURI MOROGORO.

Mshambulia wa Polisi Morogoro Nohoda Bakari akiwania dhidi ya mlinzi wa African Lyon ya Jijini Dar es Salaam, Hood Mayanja kulia wakati wa mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo katika mchezo huo African Lyon ilikubali kipigo cha bao 1-0 na kuendelea kuburuza mkia katika mzunguko huu wa pili wa ligi hiyo.
 Mlinda Mlango wa African Lyon Abdul Seif kulia akidaka mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Polisi Morogoro Keneth Masumbuko wakati wa mchezo wao.
 Mlinzi wa African Lyon Ibrahim Issac kulia akipiga mahesabu ya kumzuia mshambuliaji wa Polisi Morogoro Tizo Chomba kushoto.
Mshambuliaji wa Polisi Morogoro Keneth Masumbuko ambaye alikuwa akisumbua ngome ya African Lyon kushoto akimtoka mlinzi wa timu hiyo Ibrahim Issac ili  kupeleka mashambulizi katika lango wa wapinzania wao.
  Askari wa kuliza ghasia wakiwa wanawapa ulinzi waamuzi wa mchezo huo chini ya mwamuzi wa kati Andrew Shamba wa Pwani mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao wenyewe waliibuka na ushindi wa bao 1-0.
 Benchi la ufundi la African Lyon likiongozwa na kocha mkuu Charles Otien wa kwanza kushoto wakati wakishuhudia jahazi likizama dhidi ya maafande wa Polisi Morogoro kwa kukubali kutwandikwa bao 1-0.
 Benchi la ufundi la Polisi Morogoro chini ya kocha mkuu wa timu hiyo Mohamed Richard wa pili kutoka kushoto ambapo walifanikiwa kuliongoza vema jahazi lao dhidi ya African Lyon na kuibua kidedea kwa bao 1-0.
 KIKOSI CHA AFRICAN LYON.
 KIKOSI CHAPOLISI MOROGORO.

 Wachezaji wa polisi Morogoro wakiwasalimia wachezaji wa African Lyon muda mfupi kabla ya kuanza mchezo wao.
 Hapa waamuzi wakiwaongoza wachezaji kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kuingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo huo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: