KWA UFUPI
“Tumeshindwa kufikia mwafaka kutokana na viongozi wa dini ya Kiislamu kutoa masharti ambayo yapo nje ya uwezo wetu. Hivyo kikao hiki tunakihairisha kwa muda kutoa fursa kwa Waislamu kufanya majadiliano ili kupata mwafaka na wakikubaliana, Serikali ipo tayari kuendelea na majadiliano,”
WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA.
VIONGOZI wa dini ya Kiislamu mkoani Geita wamesusia kikao cha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kusuluhisha mgogoro wa uchinjaji baina yao na viongozi wa dini ya Kikristo.
Viongozi hao wametoa masharti ya kuachiwa wenzao sita waliokamatwa kuhusiana na mauaji ya mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Buseresere, Mathayo Kachila (45).
Kikao hicho ambacho kilidumu kwa muda wa dakika 45, kilivunjika baada ya viongozi wa Waislamu kutaka kuachiwa kwa wafuasi wao baada ya wafuasi wa dini ya Kikristo kuachiwa baada ya vurugu zile.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada viongozi hao kuondoka,

Pinda alisema kikao chake kimeshindikana kutokana na viongozi wa dini ya Kiislamu kutoa masharti ambayo yapo nje ya uwezo wake.
“Tumeshindwa kufikia mwafaka kutokana na viongozi wa dini ya Kiislamu kutoa masharti ambayo yapo nje ya uwezo wetu.
Hivyo kikao hiki tunakihairisha kwa muda kutoa fursa kwa Waislamu kufanya majadiliano ili kupata mwafaka na wakikubaliana, Serikali ipo tayari kuendelea na majadiliano,”alieleza.
Hivyo kikao hiki tunakihairisha kwa muda kutoa fursa kwa Waislamu kufanya majadiliano ili kupata mwafaka na wakikubaliana, Serikali ipo tayari kuendelea na majadiliano,”alieleza.
Katika kikao cha usuluhishi kama hicho kilichofanyika Mwanza, Pinda alieleza kuwa wakileta masharti ya wenzao waliokamatwa kuachiwa itakuwa vigumu kwa vile hata mmiliki wa bucha huko Buseresere hajakamatwa na kuongeza kuwa zipo tuhuma za kutumika silaha wakati wa vurugu hizo.
Baada ya kutoka nje ya kikao, Waislamu waliondoka eneo la kikao na viongozi wa Kikristo nao walitoka na kufanya kikao katika moja ya makanisa kujadiliana hatima yao.
0 comments:
Post a Comment