BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JESHI LA POLISI MORO LAHAHA KUMSAKA ASKARI WA HIFADHI YA WANYAMAPORI YA MIKUMI KWA TUHUMA ZA KUMPIGA RISASI MFUGAJI.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MOROGORO FAUSTINE SHILOGILE.

Na Juma Mtanda.
JESHI la polisi mkoa wa Morogoro lipo katika wakati mgumu wa kumsaka askari wa hifadhi ya taifa ya wanyamapori ya Mikumi kwa tuhuma za kufyatua risasi iliyomlenga mfugaji, Muri Sityo (23) kisogoni na kufariki dunia papo hapo kisha mwili wake kutupwa sehemu ambayo haijajulikana mkoani Morogoro.

Tukio hilo linadaiwa kutokea marchi 1 mwaka huu majira ya saa 6 mchana wakati mfugaji huyo akinywesha maji mifugo na wenzake katika bwawa lililopo ndani ya hifadhi hiyo jirani na mpaka wa kijiji cha Mkata-Luhoza wilaya ya Kilosa mkoani hapa.

Akizungumza na gazeti hili katikati ya wiki mjini hapa katika mahojiano maalum, Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alisema kuwa ni kweli jeshi la polisi linamska askari wa hifadhi ya taifa ya wanyamapori ya Mikumi kwa tuhuma za kufyatua risasi na kusababisha kifo cha mfugaji, Muri Sityo kufariki dunia papo hapo marchi 1 mwaka huu mkoani hapa.

Shilogile alisema kuwa jeshi la polisi hivi sasa lipo katika uchunguzi wa kina wa tukio hilo kwa kumsaka askari na pamoja na kuchukua sampori ya tope lililochanganyikana na damu kwa ajili ya kupimwa kwa mkemia mkuu wa serikali ili kuweza kubaini ukweli wa tukio hilo ambalo mpaka sasa limekubikwa na utata kutokana na mazingira ya tukio lenyewe ikiwemo mwili wa marehemu kutokutwa eneo la tukio .

Nilituma askari kwenda eneo la tukio lakini walipofika hawakuweza kuona mwili wa marehemu na badala yake waliona damu iliyotapakaa katika tope hivyo walichukua tope lenye damu kwa ajili ya uchunguzi zaidi pamoja na kumsaka mtuhumiwa” alisema Shilogile.

Aliongeza kwa kusema kuwa jeshi la tayari limeanza uchunguzi wa awali ikiwemo kuwahoji askari waliokuwa katika Mbogayaga Ranger Post iliyopo jirani na mpaka wa kijiji Mkata-Luhoza na hifadhi hiyo.

Akizungumzia juu ya kutokamatwa kwa mtuhumiwa huyo mpaka sasa, Shilogile alisema kuwa juhudi zinaendelea kufanywa zikiwemo za kufanya mazungumzo na mkuu wa hifadhi ya taifa ya Mikumi na kati ya makubaliano yaliyofikiwa ni lazima mkuu huyo anapaswa kumfikisha mtuhumiwa katika mikono ya jeshi la polisi Morogoro. Alisema Shilogile.

Shilogile aliendelea kueleza kuwa taarifa alizonazo juu ya mtuhumiwa huyo ni kuwa yupo likizo jambo ambalo linawapa kazi katika harakati za kumkamata mtuhumiwa.

Shilogile alimetoa wito kwa taasisi za zinazohusika na ulinzi ikiwemo na jeshi la polisi kiujumla kuzingatia zaidi sheria pindi wanamkamata mtuhumiwa kuhakikisha anafikishwa salama katika vyombo vya dola ili sheria ifuate mkondo wake huku akiwataka wananchi nao kuzingatia sheria za nchi bila shuruti ili mkoa wa Morogoro na Tanzania kiujumla uendelea kuwa na amani.

Katika tukio hilo ambalo lilitokea majira ya saa 6 mchana mwaka huu ndani ya hifadhi ya taifa ya wanyamapori Mikumi askari wenye cheo cha sajeti (Pius Minja) anadaiwa kufyatulia risasi na kumpiga mfugaji, Muri Sityo (23) kisogoni na kufariki dunia papo hapo wakati yeye (marehemu) akimwesha mifugo maji mifugo bwawa lililopo ndani ya hifadhi hiyo katika mpaka na kijiji cha Mkata-Luhoza kata ya Tindiga Kilosa Morogoro.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: