BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE WA JIMBO LA MORO MJINI KUTUMIA SH 24O MILIONI KUCHIMBA VISIMA VYA MAJISAFI NA SALAMA.


Katibu wa mbunge wa jimbo la Morogoro mjini abdullaziz Abood, Mourice Massala wa kwanza kushoto akisimamia zoezi la kutekaji wa maji kwa wakazi wa eneo la Ninja baada ya kuchimbwa kisima ambapo zoezi lilifanyika kabla ya kukabidhi kisima kwa uongozi wa eneo hilo mkoani Morogoro.
 Picha na Blog JumaMtanda.blogspot.com



MBUNGE wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood anatarajia kutumia zaidi ya sh 240 Milioni kwa ajili ya kutatua kero ya maji katika kata tano yenye kero ya maji kwa kuchimba visima vya majisafi na salama katika Manispaa ya Morogoro.

Kati ya kata hizo tano kata ya Kihonda ndiyo yenye changamoto kubwa ya uhaba wa upatikanaji wa majisafi na salama na kuwa mpango wa kuchimba visima vya maji katika kata hizo itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua kero ya majisafi na salama kwa wananchi wa maeneo hayo.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili mjini hapa, Abood alisema kuwa zaidi ya sh 240 anataraji kutumia kwa ajili ya kuchimba visima katika kata hizo ili kupunguza changamoto ya maji hasa baada ya kata hizo sehemu nyingi ambazo zipo pembezoni mwa Manispaa ya Morogoro zimekuwa hajafikiwa na miundombinu ya mamlaka ya majisafi na majitaka (Moruwasa) tangu kata hizo zimeundwa.

Abood alisema kuwa mpaka sasa kuna visima 25 ambavyo tayari vimechimbwa kutokana na mahitaji  katika kata hizo ikiwemo Kihonda, Mkundi, Tungi, Kichangani na Mzinga ambavyo visima hivyo vimechimbwa katika maeneo yenye shida ya upatikanaji wa maji katika awamu mbili.


“Kuna visima 25 tayari wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama katika maeneo yote yenye kero kubwa ya changamoto ya upatikanaji wa maji na kuwa uchimbaji wa visima hivyo umetokana na ukweli kuwa mpaka sasa baadhi ya kata hizo bado hazijapata miumbombinu ya mamlaka ya majisafi na majitaka ndiyo maana nimechimba visima hivyo” alisema Abood.

Abood aliyataja maeneo hayo ambayo yana kero kubwa ya upatikanaji wa majisafi na salama katika Manispaa ya Morogoro kuwa ni pamoja na Mzinga, Areasix, Lukobe, Tungi, Mkundi, Kichangani na Areafive na kuwa tayari kiasi cha sh 134 Milioni zimetumika katika awamu mbili ambao awamu ya kwanza vimechimbwa visima 10 na awamu ya pili visima 15 vinaendelea kuchimbwa katika kata hizo.

Baadhi ya maeneo hayo miundombinu ya mamlaka hiyo haijawafikia na kuwa kumekuwa na mgao unaosababisha wakazi wake maeneo hayo kukumbwa na uhaba mkubwa wa maji kwa muda mrefu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: