Kwa ufupi
Mabingwa watetezi, Simba wakiwa wanachechemea
wanashuka kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kuivaa Toto African leo
wakati vinara Yanga wakiwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kuivaa
Polisi Morogoro katika harakati za kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania
Bara.Wachezaji wa Toto Africans, wakiwa wamembeba juu kocha wao baada ya
kuifunga Simba katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza kwenye
Uwanja wa Taifa. Picha na Michael Matemanga.
DAR ES SALAAM.
Mabingwa watetezi, Simba wakiwa wanachechemea wanashuka kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kuivaa Toto African leo wakati vinara Yanga wakiwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kuivaa Polisi Morogoro katika harakati za kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba inashuka uwanjani baada ya kufungwa bao 1-0
na Kagera Sugar katika mchezo uliopita na kubaki nafasi ya tatu ikiwa na
pointi 34 sawa wa vijana hao wa Kagera ambao leo wataivaa Mtibwa Sugar.
Yanga inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 48
itakuwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ikicheza na Polisi Moro huku Azam FC
inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 40 ikipepetana na Ruvu
Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini Mlandizi.
Kocha wa Yanga, Ernie Brandts amesema
wataishambulia Polisi Moro kama nyuki kwa lengo la kushinda mchezo huo
na kubakiza dakika 270 (Mechi tatu) kabla ya kutawazwa mabingwa wapya wa
ligi hiyo.
Iwapo Yanga itashinda mchezo huo itafikisha pointi
51 na kubakiza pointi tisa tu ambazo ni sawa na mechi tatu kabla ya
kutwaa ubingwa wa ligi na kukata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika
mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Yanga ikiwa inawaza ushindi na kutwaa ubingwa,
wenyeji wao Polisi watakuwa wakihaha kushinda mchezo huo kukimbia balaa
la kushuka daraja.
“Binafsi nafikiri mchezo utakuwa mgumu, kila mtu
anapaswa kulifahamu hilo,” alisema kocha Brandts. “Kwa upande wetu
tumejipanga vya kutosha kukabiliana nao, lakini hatupaswi kuidharau hata
kidogo Polisi,” alisisitiza kocha Brandts.
Naye beki wa Polisi Moro, Chacha Marwa amesisitiza kucheza kwa bidii na kijituma kwa lengo la kuitibulia Yanga kileleni.
“Kwa upande wetu tumejiandaa vya kutosha
kukabiliana na Yanga,” alisema beki huyo wa zamani wa Moro United,
Mtibwa Sugar na Yanga.
Jijini Mwanza, Simba nao watakuwa na kibarua
kigumu pia, kwani watakuwa wakicheza na Toto inayosaka kujinasua na
janga la kushuka daraja.
Kocha wa Simba, Patrick Liewig alisema anajua
matokeo mabaya waliyoyapata kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Kagera
Sugar yatawafanya wachezaji wake wacheze kwa presha kubwa.
“Nimewaambia wachezaji kuwa Toto itatupania kwa sababu inasaka pointi tatu muhimu tena ikiwa kwao.
0 comments:
Post a Comment