BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAHAKAMA YATUPA MAOMBI KESI YA UCHAGUZI KENYA.

Kwa ufupi
Kazi ya kuhesabu upya kura za urais kutoka vituo vya kupigia kura 22 ilianza mapema jana chini ya ulinzi mkali baada wa mawakala wa Muungano wa Cord na Jubilee kuapishwa.
http://www.mwananchi.co.tz
 RAILA ODINGA AKIPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA KENYA.
 UHURU KENYATTA AKIPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA KENYA.
NAIROBI.  
MAHAKAMA ya Juu (Supreme Court) nchini Kenya jana ilitupilia mbali viapo viwili katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta wa Muungano wa Jubilee.
Maombi yaliyotupwa ni lile la muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali lililoitaka mahakama iamuru tume ya uchaguzi kufikisha mahakamani hapo nyaraka zote zilizotumika wakati wa uchaguzi huo.
Kadhalika mahakama hiyo ilitupilia mbali hati ya kiapo yenye kurasa 839 kilichowasilishwa na upande wa Muungano wa Cord ambacho kilidai kwamba kura katika majimbo 120 zilikuwa haziwiani na idadi ya wapigakura, hivyo kuitaka mahakama hiyo iitishe uchunguzi wa kina kwa daftari hilo pamoja na kura zilizopigwa.
Katika kiapo cha Cord, Jaji Phillip Tunoi alisema kwa mujibu wa sheria hati za kiapo si haki ya mlalamikaji au mlalamikiwa hivyo kabla wa kuwakilishwa walalamikaji walipaswa kupata ruhusa ya mahakama, jambo ambalo halikufuatwa.
Kwa upande wake Jaji Mohammed Warsame aliyesoma uamuzi dhidi ya kiapo cha mashirika yasiyokuwa ya kiserikali alitupilia mbali maombi yao kwa maelezo kwamba yalifikishwa mahakamani nje ya muda uliowekwa kisheria.
Katika ombi lao muungano huo wa Africog ulidai kuwa kufeli kwa mfumo wa kielectronikiwa kuhesabu kura ulikuwa umepangwa kwa madhumuni ya kuiba kura. Hivyo tume hiyo iamuriwe kuleta mahakamani hapo nyaraka zote ili zifanyiwe uchunguzi wa kitaalamu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: