BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE JIMBO LA MOROGORO KUSINI ATOA MASHINE 20 ZA KUVUTAA MAJI KWA VIKUNDI 12 VYA UZALISHAJI MALI. MWAG

Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Innocent Kalogeries kushoto akimwangalia msaidizi wake, Hamidu Saidi wakati akiwasha jenereta za kuvuta maji 20 ambazo ofisi yake zimewakopesha vikundi 12 vya uzalishaji wa chakula na bustani katika jimbo hilo yenye thamani ya sh 9Milioni katika kijiji cha Sesenga kata ya Mngazi ambavyo vikundi vya Umoja, Kazi Kwanza, Twidie vilinufaika na mpango huo.
 
Hapa akizungumza na wanavikundi vya Umoja, Kazi Kwanza, Twidie kata ya Mngazi.

 
Baadhi ya wanavikundi vya ujasiliamali vya uzalishaji mazao ya chakula na bustani wakiwa wamebeba mashine hizo baada ya kukopeshwa na ofisi ya mbunge wa jimbo hilo Innocent Kalogeries.
Mwanavikundi wa kikundi cha Wazee Mvuha akiwangilia maji katika kitalu kilichopandwa mbegu za mchicha ambapo kazi hiyo itakuwa imepungua kutokana na kupata mashine za kuvuta maji kwa ajili ya shughuli za kilimo, mazao ya chakula na bustani
Mmoja wa mwanakikundi cha Wazee akiwa mabeba keni yenye maji mara baada ya kuchota maji katika mto Mvuha ambapo kazi hiyo itakuwa imerahishishwa baada ya kupata mashine ya kuvuta maji.
Mbunge huyo akizungumza jambo na wanavikundi vinne vya Muungano wa Wazee wa Mvuha, Tulo Tushikamane, Tujikwamue na Tushirikiane Kongwa vyote kutoka kata ya Mvuha.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Morogoro Vijijini Salum Jazzaa akifafanua jambo juu ya ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 huku Mbunge wa jimbo hilo Innocent Kalogeries anayenong'oneza na Mwenyekiti wa kijiji cha Mtamba Paul Mtamani na kulia ni Diwani wa Kisemu Hamza Mfaume.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Morogoro Vijijini Salum Jazza akimkabidhi mmoja wa wanavikundi katika kata ya Mngazi huku mbunge wa jimbo Innocent Kalogeries kulia akishuhudia kijiji cha Sesenga.

Na Juma Mtanda, Morogoro.
MBUNGE wa jimbo la Morogoro Kusini, Innocent Kalogeries amewataka wanachama wa vikundi vya wajaliamali kuongeza juhudi za uzalishaji mazao ya chakula na bustani baada ya mfuko wa jimbo hilo kutoa mkopo wa mashine 20 za kuvuta maji zenye thamani ya sh 9milioni katika jimbo hilo mkoani hapa.

Akizungumza na wanavikundi 242 kwa nyakati tofauti katika jimbo hilo mkoani hapa, Kalogeries alisema kuwa  jumla ya vikundi 12 vimepatiwa mkopo wa mashine 20 za kuvuta maji kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na bustani lengo likiwa kuendeleza juhudi za mkoa wa Morogoro kuwa ghala la chakula.

Kalogeries alisema kuwa lengo la kutoa mkopo huo kwa vikundi hivyo ni mwendelezo wa ahadi ya utekelezaji wa ilani ya ccm wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ya kuwawezesha wananchi katika harakati za kuwakwamua katika dimbwi la umasikini na kufanya mkoa wa Morogoro unakuwa ghala la chakula.

“Mfuko wa jimbo la Morogoro kusini umetumia kiasi cha sh 9milioni kwa ajili ya ununuzi wa mashine 20 za kuvuta maji ambapo sasa mutakuwa na uwezo wa kulima mazao ya chakula na bustani mwaka mzima lakini mashine hizi zitunze ikiwemo na kulipa kiasi cha marejeshi ya sh45,000 baada ya miezi sita ili na vikundi vingine viweze kukopeshwa”. Alisema Kalogeries.

Vikundi vilivyofaidika na mkopo huo wa mashine za kuvuta maji ni pamoja na Muungano wa Wazee wa Mvuha, Tulo Tushikamane, Tujikwamue na Tushirikiane Kongwa vyote kutoka kata ya Mvuha, Tushirikiane Group kutoka kata ya Bwakila Chini na Polepole Tugendege kata ya Bwakila Juu.

Alivitaja vikundi vingine kuwa ni Jitihada Ufike Vegetable Group kata ya Kinole, Umoja, Kazi Kwanza, Twidie kutoka kata ya Mngazi, Mshikamano, Kiwamamo vya kata ya Kisaki vyote vikiwa na jumla ya wananchama 242 kutoka katika vikundi 12 katika tarafa ya Matombo, Mvuha na Kisaki katika halmashauri hiyo ya wilaya ya Morogoro.

Kalogeries alisema kuwa baada ya mfuko huo wa jimbo kutumia kiasi hicho cha sh 9milioni kwa vikundi vya mazao ya chakula na bustani kazi iliyopo mbele yake ni kuwashawishi vijana wanaojishughulisha na kutafuta kipato kwa kuendesha pikipiki maarufu (Bodaboda) kujiunga katika vikundi ili nao wawezeshe kupokopeswa pikipiki.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: