KENYATTA MBWAGA ODINGA UCHAGUZI MKUU WA KENYA 2013.
MWANA wa kiume wa muasisi wa taifa la Kenya, Uhuru Kenyatta, ameshinda
uchaguzi wa rais kwa asilimia 50.07 ya kura kwa mujibu wa matokeo
yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi na hivyo kuepuka marudio ya uchaguzi.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Isaack Hassan Mwenyekiti wa tume ya
uchaguzi amesema Kenyatta amejipatia asilimia 50.07 ya kura ambazo ni
kura milioni 6.13 kulinganishwa na kura milioni 5.3 alizopata mpinzani
wake Raila Odinga.Kutokana na matokeo hayo Hassan amemtangaza rasmi
Kenyatta kuwa rais mteule wa Kenya.
Kenyatta anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu kufuatia uchaguzi wa Kenya wa mwaka 2007 uliozusha umwagaji damu wa kikabila.
Baada ya kuibuka kwa matokeo ya awali leo alfajiri wafuasi wa Kenyatta wenye furaha walimiminika katika mitaa ya Nairobi na katika miji yenye wafuasi wake wakuu wa kikabila wakishehereka kwa kuwasha fataki na kupeperusha matawi ya miti huku wakiimba: "Uhuru, Uhuru, Uhuru!"
Jumuiya ya kimataifa na ushindi wa Uhuru
Marekani na mataifa mengine ya magharibi yalisema kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo kwamba ushindi wa Kenyatta utafanya uhusiano wa kidiplomasia na nchi hiyo kuwa mgumu ambayo ni mshirika muhimu katika vita dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali za Kiislam katika kanda hiyo.
Mwanadiplomasia mmoja wa mataifa ya Magharibi amesema kwamba halitokuwa tatizo iwapo Kenyatta atatowa ushirikiano wake kwa mahakama ya ICC na kwamba wanaheshimu uamuzi wa wapiga kura walio wengi nchini Kenya.
Vipi serikali za nchi za Magharibi zitaishughulikia Kenya chini ya utawala wa Kenyatta na kwa kiasi gani zitakuwa tayari kushikiana na serikali yake itategemea sana jinsi Kenyatta mwenyewe na mgombea mwenza wake William Ruto ambaye pia anashtakiwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC watakavyotowa ushirikiano wao kwa mahakama hiyo.
Wote wawili Kenyatta na Ruto wamesema kwamba watajitahidi kusafisha majina yao juu ya kwamba Kenyatta ilibidi azime vijembe vya Odinga wakati wa kampeni kwamba itabidi aongoze serikali kwa kutumia Skype kutoka The Hague makao makuu ya mahakama ya ICC.
Lakini hali ya wasi wasi imetanda katika mji wenye wafuasi
wengi wa mpizani wa Kenyatta Waziri Mkuu Raila Odinga ambaye yuko nyuma
ya Kenyatta baada ya kujipatia asilimia 43.28 ya kura.
Wafuasi wake walikuwa wakipiga mayowe kwamba "bila ya Raila hakuna amani" huku vikosi vya usalama vikiangalia huko Kisumu ambapo kulizuka ghasia kufuatia uchaguzi wa mwaka 2007.
Mshauri wa karibu wa Odinga ambaye alishindwa katika uchaguzi wa mwaka 2007, Salim Lone, amesema mgombea wake hatoyakubali matokeo hayo na atawasilisha pingamizi la sheria mahakamani.
Akizungumza kwa niaba ya Odinga kabla ya kutangazwa kwa matokeo ameliambia shirika la habari la Uingereza Reuters kwamba Odinga hakubali matokeo hayo ya uchaguzi na kwamba iwapo Uhuru Kenyatta anatangazwa kuwa rais mteule moja kwa moja atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Kambi ya Odinga imesema wakati kura zilipokuwa zikihesabiwa kwamba kuhesabiwa kwa kura kulikuwa na kasoro kubwa sana na kutaka usitishwe. Lakini imeahidi kushughulikia mizozo yoyote ile katika mahakama na sio barabarani.
Wakenya wanatarajia uchaguzi huu ambao hadi sasa umepita salama na kuwepo kwa vurugu kidogo tu wakati wa siku ya kupiga kura utarudisha sifa ya nchi hiyo kama mojawapo ya taifa lenye demokrasia imara barani Afrika baada ya vurugu za baada ya uchaguzi kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,200 hapo mwaka 2007.
Wakenya wengi wamesema wameazimia kuepuka marudio ya vurugu za
baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambazo ziliukwamisha uchumi wa nchi
hiyo.
Viongozi wa makanisa huko Kisumu magharibi ya Kenya ambapo miaka mitano iliopita uliathirika vibaya safari hii wamechukuwa juhudi za kuondowa hali ya mvutano.
Waangalizi wa kimataifa kwa kiasi kikubwa wamesema kwamba uchaguzi huo na zoezi la kuhesabu kura vimefanyika kwa uwazi hadi sasa na tume ya uchaguzi ambayo imechukuwa nafasi ya ile ya zamani iliopoteza sifa iliahidi kuwepo kwa uchaguzi wa kuaminika.
Ili kuweza kushinda duru ya kwanza, mgombea alikuwa anahitajika kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura.
Ushindi huo wa duru ya kwanza unamaanisha kwamba Wakenya waliokuwa wamesubiri kwa siku tano kujuwa matokeo hivi sasa hawatokuwa na duru ya pili ya uchaguzi ambayo ingeongeza hali ya wasi wasi nchini humo.
Pande zote mbili zimekuwa zikitegemea mno makundi yao ya kikabila katika taifa ambapo utiifu wa kikabila mara nyingi umekuwa juu kuliko itikadi wakati wa kupiga kura.
Kenyatta ni Mkikuyu ambalo ni kabila kubwa nchini Kenya, Odinga ni Mjaluo. Wote waili wana wagombea wenza kutoka makabila mengine.
Wakenya wengi wanasema uchaguzi huu ulikuwa na uwazi zaidi.
Idadi ya watu iliojitokeza kupiga kura ni asilimia 86 kati ya watu milioni 14.3 waliostahiki kupiga kura.
Kenyatta anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu kufuatia uchaguzi wa Kenya wa mwaka 2007 uliozusha umwagaji damu wa kikabila.
Baada ya kuibuka kwa matokeo ya awali leo alfajiri wafuasi wa Kenyatta wenye furaha walimiminika katika mitaa ya Nairobi na katika miji yenye wafuasi wake wakuu wa kikabila wakishehereka kwa kuwasha fataki na kupeperusha matawi ya miti huku wakiimba: "Uhuru, Uhuru, Uhuru!"
Jumuiya ya kimataifa na ushindi wa Uhuru
Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wakishangiria ushindi wa kiongozi wao.
Kufuatia kutangazwa kwake na Tume ya Uchaguzi kuwa mshindi wa
uchaguzi huo Kenya inakuwa nchi ya pili ya Afrika baada ya Sudan kuwa na
rais aliyeko madarakani anayekabiliwa na mashataka katika mahakama ya
kimataifa ya uhalifu ya ICC yenye makao yake huko The Hague nchini
Uholanzi.Marekani na mataifa mengine ya magharibi yalisema kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo kwamba ushindi wa Kenyatta utafanya uhusiano wa kidiplomasia na nchi hiyo kuwa mgumu ambayo ni mshirika muhimu katika vita dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali za Kiislam katika kanda hiyo.
Mwanadiplomasia mmoja wa mataifa ya Magharibi amesema kwamba halitokuwa tatizo iwapo Kenyatta atatowa ushirikiano wake kwa mahakama ya ICC na kwamba wanaheshimu uamuzi wa wapiga kura walio wengi nchini Kenya.
Vipi serikali za nchi za Magharibi zitaishughulikia Kenya chini ya utawala wa Kenyatta na kwa kiasi gani zitakuwa tayari kushikiana na serikali yake itategemea sana jinsi Kenyatta mwenyewe na mgombea mwenza wake William Ruto ambaye pia anashtakiwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC watakavyotowa ushirikiano wao kwa mahakama hiyo.
Wote wawili Kenyatta na Ruto wamesema kwamba watajitahidi kusafisha majina yao juu ya kwamba Kenyatta ilibidi azime vijembe vya Odinga wakati wa kampeni kwamba itabidi aongoze serikali kwa kutumia Skype kutoka The Hague makao makuu ya mahakama ya ICC.
Kisumu kuna wasiwasi
Wafuasi wake walikuwa wakipiga mayowe kwamba "bila ya Raila hakuna amani" huku vikosi vya usalama vikiangalia huko Kisumu ambapo kulizuka ghasia kufuatia uchaguzi wa mwaka 2007.
Mshauri wa karibu wa Odinga ambaye alishindwa katika uchaguzi wa mwaka 2007, Salim Lone, amesema mgombea wake hatoyakubali matokeo hayo na atawasilisha pingamizi la sheria mahakamani.
Akizungumza kwa niaba ya Odinga kabla ya kutangazwa kwa matokeo ameliambia shirika la habari la Uingereza Reuters kwamba Odinga hakubali matokeo hayo ya uchaguzi na kwamba iwapo Uhuru Kenyatta anatangazwa kuwa rais mteule moja kwa moja atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Kambi ya Odinga imesema wakati kura zilipokuwa zikihesabiwa kwamba kuhesabiwa kwa kura kulikuwa na kasoro kubwa sana na kutaka usitishwe. Lakini imeahidi kushughulikia mizozo yoyote ile katika mahakama na sio barabarani.
Wakenya wanatarajia uchaguzi huu ambao hadi sasa umepita salama na kuwepo kwa vurugu kidogo tu wakati wa siku ya kupiga kura utarudisha sifa ya nchi hiyo kama mojawapo ya taifa lenye demokrasia imara barani Afrika baada ya vurugu za baada ya uchaguzi kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,200 hapo mwaka 2007.
Wakenya waazimia amani
Viongozi wa makanisa huko Kisumu magharibi ya Kenya ambapo miaka mitano iliopita uliathirika vibaya safari hii wamechukuwa juhudi za kuondowa hali ya mvutano.
Waangalizi wa kimataifa kwa kiasi kikubwa wamesema kwamba uchaguzi huo na zoezi la kuhesabu kura vimefanyika kwa uwazi hadi sasa na tume ya uchaguzi ambayo imechukuwa nafasi ya ile ya zamani iliopoteza sifa iliahidi kuwepo kwa uchaguzi wa kuaminika.
Ili kuweza kushinda duru ya kwanza, mgombea alikuwa anahitajika kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura.
Takwimu za kura
Takwimu za tume ya uchaguzi zimeonyesha kwamba Kenyatta
ameshinda kura 6,173,433 kati ya jumla ya kura 12,338,667
zilizopigwa.Odinga amejipatia kura 5,340,546.Ushindi huo wa duru ya kwanza unamaanisha kwamba Wakenya waliokuwa wamesubiri kwa siku tano kujuwa matokeo hivi sasa hawatokuwa na duru ya pili ya uchaguzi ambayo ingeongeza hali ya wasi wasi nchini humo.
Pande zote mbili zimekuwa zikitegemea mno makundi yao ya kikabila katika taifa ambapo utiifu wa kikabila mara nyingi umekuwa juu kuliko itikadi wakati wa kupiga kura.
Kenyatta ni Mkikuyu ambalo ni kabila kubwa nchini Kenya, Odinga ni Mjaluo. Wote waili wana wagombea wenza kutoka makabila mengine.
Wakenya wengi wanasema uchaguzi huu ulikuwa na uwazi zaidi.
Idadi ya watu iliojitokeza kupiga kura ni asilimia 86 kati ya watu milioni 14.3 waliostahiki kupiga kura.
0 comments:
Post a Comment