Kwa ufupi
Akizungumza jana katika uzinduzi wa Chadema kwa
Kanda ya Kati, Mbowe alisema Spika Makinda amekuwa ni mwongo hata
kuidanganya dunia kuwa uamuzi wao ni sahihi jambo ambalo si kweli.
http://www.mwananchi.co.tzMbowe akiwa na wanachama wa Chadema mjini Dodoma.
http://www.mwananchi.co.tzMbowe akiwa na wanachama wa Chadema mjini Dodoma.
DODOMA:
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewasifu wabunge wa chama hicho waliosimamishwa huku akimshambulia Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai kuwa wanaliendesha Bunge kiharamia.
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewasifu wabunge wa chama hicho waliosimamishwa huku akimshambulia Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai kuwa wanaliendesha Bunge kiharamia.
Akizungumza jana katika uzinduzi wa Chadema kwa
Kanda ya Kati, Mbowe alisema Spika Makinda amekuwa ni mwongo hata
kuidanganya dunia kuwa uamuzi wao ni sahihi jambo ambalo si kweli.
“Spika Makinda ni mwongo, ameidanganya dunia na
amekuwa akitumia maneno ya uongo kuhalalisha uharamia uliofanywa na
Naibu Spika wa Bunge kwa kuwatoa ndani wabunge watano wa
Chadema,”alisema na kuongeza.
“Uhuni kama huu ndugu zangu haukubaliki,
tutaendelea kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunatetea masilahi
ya nchi hii na watu wake.
Na hapa natangaza mbele yenu kuwa wabunge walioondolewa ndani ya Bunge ni mashujaa,” alisisitiza Mbowe.
Na hapa natangaza mbele yenu kuwa wabunge walioondolewa ndani ya Bunge ni mashujaa,” alisisitiza Mbowe.
Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, aliwaambia wanachama na mashabiki wa Chadema kuwa
wanafanya kazi katika mazingira magumu ndani ya Bunge na kwamba
wanatakiwa kuwa majasiri wakiwa bungeni.
Alisema kwamba wakati wote wamekuwa wakishutumiwa
kuwa wanafanya fujo ndani ya Bunge, jambo alilosema siyo kweli bali wao
wanasimamia Kanuni za Bunge ambazo zimekuwa zikivunjwa na Spika na Naibu
wake kila wanapokuwa ndani ya viti vyao.
Alisisitiza kuwa hawako tayari na kamwe hawatakuwa
tayari kutii mamlaka yoyote wanayoamini kuwa inawakandamiza na
kuwaondolea haki yao, zaidi ya kupambana.
Kiongozi huyo alinukuu baadhi ya vifungu vya
Kanuni za Bunge alivyosema kuwa vingetumika kwa kumaliza tatizo la
Lissu, aliyemwelezea kuwa alikuwa sahihi, hata angesimama mara mia moja
kwa sababu alikuwa akipinga upuuzi.
Kuhusu Katiba
Akizungumzia masuala ya mchakato wa Katiba Mpya,
Mbowe alisema kuwa uamuzi uliotolewa ndani ya Bunge katika hotuba yake
ndiyo msimamo wa Chadema, akatahadharisha kuwa ikiwa Serikali
haitakubali kufanya marekebisho waliyopendekeza, chama hicho kitajitoa.
“Ule ulikuwa ni msimamo wa Kamati Kuu ya chama
chetu na bado tunasisitiza kuwa wasipokuwa makini tutajitoa. Kama noma
na iwe noma, hata kama uchaguzi, tutashinda kwa nguvu ya Mungu,” alisema
na kushangiliwa na umati wa watu.
Hata hivyo, alionya kuwa kama Serikali itapuuza
ushauri wao, itaisoma namba kwa kuwa wanajua kinachotaka kufanywa na
tayari wameshajipanga kukabiliana nacho.
0 comments:
Post a Comment