BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DIWANI AMTANDIKA MANGUMI KATIBU WA CCM MORO.


 
MWENYEKITI MPYA WA CCM MOROGORO, INNOCENT KALOGERIS AKITAFARI JAMBO MARA BAADA YA KUSHINDA NAFASI. 

Na Juma Mtanda, Morogoro.
KATIBU wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, Stanford Mndoda amedai kupigwa magumi na mateke katika sehemu mbalimbali za mwili wake diwani wa kata hiyo akishirikiana na mfanyabiashara maarufu baada ya kumtuhumu kufanya kampeni za udiwani kwa mtu anayedhaniwa kuwa anaweza kugombea nafasi ya udiwani katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 mkoani hapa.



Akizungumza na gazeti hili katika ofisi za gazeti hili mjini hapa, Katibu wa chama hicho, Stanford Mndoda alisema kuwa amepokea kipigo kutoka kwa diwani wa kata hiyo akishirikiana na mfanyabishara maarufu aliyefahamika kwa jina la Augostino Simba Magwila katika tukio ambalo linadaiwa kufanyika ofisi za mfanyabiashara huyo mtaa wa Shamba majira ya saa 9 alasiri marchi 30 mwaka huu baada ya kufunga mlango wa ofisi hiyo.

Mndoda alisema kuwa kabla ya kumpata mkasa huo alipigiwa simu na mfanyabiashara huyo majira ya saa 8:45 mchana na kuelezwa kuwa kufika ofisini kwake kwani ana shida naye na baada ya kufika ofisini kwane majira ya saa 9 alasiri alimkuta yeye na diwani wa kata ya Kiwanja cha Ndege, Mohamed Matikula ndani ya ofisi hiyo.

“Nilipigwa mateke na mangumi kichwani, tumboni na mgongoni na Augostino Simba Magwila na kipigo hicho baada ya mimi kujibu swali lake alilouliza kuwa juzi (marchi 29) nilikuwa na nani, nami nikajibu kuwa nilikuwa na Adolf Bingileki ndipo kimkong’oto uliopoanza”. Alisema Mndoda.

Aliendelea kueleza kuwa alinipigia simu majira ya saa 8:45 mchana siku ya tukio na hiyo ilikuwa ya simu ya nne kupigiwa na Mgwila na alipofika ofisini kwake saa 9 alasiri.

Aliendelea kueleza kuwa baada ya kujibu swali hilo Magwila alitoa historia ya mtu ambaye alimsingizia kesi jijini Dar es Salaam na kusokwa rumande na baada ya kutoka rumande alimfuata mtu aliyemsingizia jambo kwa polisi na kumwadhibu kwa kumpiga magumu sehemu mbalimbali za mwili wake kabla ya kumbadilishia kibao Katibu huyo na kuanza kumpiga huku diwani akimkung’uta.

Kosa lililonifanya nipigwe ni kuwa na Adolf Bingileki ambaye kipindi cha nyumba aliwahi kuwa diwani wa kata hiyo hivyo madai yao wanadhani yeye kuwa na Bingileki walikuwa wakipanga mipango ya kugombea nafasi ya udiwani katika uchaguzi mkuu ujao kitu ambacho sio kweli kwani yeye ni mtu ambaye anafahamiana naye kama watu wengine. Alisema Mndoda.

Alitaja sehemu ambazo amepigwa ni kuwa kichwani, tumboni, mgongoni kwa ngumi n mateke wakishirikiana kwa pamoja ambapo baada ya kipigo hicho alijisikia maumivu na kwenda kulipoti kwa Mwenyekiti wa CCM kata hiyo ambaye alimshauri kwenda polisi ili kutoa taarifa za tukio hilo.

Baada ya kutoa taarifa katika kituo kikuu cha polisi alipewa PF-3 na kupatiwa huduma ya kwanza kabla ya kupewa RB No Mor/RB/3395/013 na kufunguliwa jalada la shambulio la kudhuru mwili katika kituo kikuu cha polisi Morogoro.

Diwani wa kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, Mohamed Matikula akizungumzia tuhuma hizo dhidi yake alikanusha kufanya tendo hilo na kusema kuwa muda uliotajwa yeye wakati huo alikuwa katika mchezo wa ligi kuu baina ya Polisi Moro SC na Yanga Afrika uwanja wa jamhuri.

Matikula alisema kuwa sio kweli na hajafanya tukio hilo kwani muda unaodaiwa kupigwa kwa Katibu wa CCM katika kata hiyo yeye alikuwa mmoja wa mashabiki wa mchezo wa soka baina ya Polisi Moro SC na Yanga uwanja wa jamhuri sasa yeye alijigawanya vipi na kudai hajaonana na kiongozi huyo siku ya tukio.

“Mimi kama nimeona amenifanyia kosa ningemshtaki katika ngazi ya chama kuanzia kata mpaka mkoa na huo ni uzushi kwani wana tabia ya kumchonganisha na wananchi”. Alisema Matikula.

Matikula alisema kuwa kumekuwa na majungu na mbinu chafu za kumchafua yeye na kudai katika uchaguzi wa mwaka 2010 alichafuliwa na kupelekewa na maafisa wa Takukuru hata hivyo madai yao yalionekana batili na niliendelea na harakati za kugombea.

Naye mfanyabiahsra aliyehamika kwa jina la Augostino Simba Magwila alijibu tuhuma hizo kwa njia ya simu asema kuwa yeye sio mwanasisa bali ni mfabiashara na asingependa kukuhusishwa na matukio ya kisiasa.

Mwandishi wa habari hizo alipotaka kujua kwanini ahusishwe na tukio hilo, Magwila alisema kuwa mwandishi sio chombo cha kusuluhisha migogoro na kueleza kuwa hapendi kufahamiani na mwandishi kwa tukio baya na kueleza kuwa katibu huyo hafahamiani naye na kuwa hayo ni majungu na kukata simu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: