Korea Kaskazini imehamisha makombora mengine kwenye mwambao wake wa
Mashariki tayari kwa mashambulizi dhidi ya Marekani, huku nchi hiyo
inayotishiwa kushambuliwa ikisema inachukua tahadhari kutokana na
vitisho hivyo.
Kulingana na chombo cha habari cha Yonhap cha Korea Kaskazini kikimnukuu
afisa mmoja wa serikali nchini humo, makombora mawili tayari
yameshasafirishwa kwa treni mapema wiki hii na kuwekwa katika magari
tayari kwa kushambulia.Kwa upande wake Wizara ya ulinzi ambayo ilithibitisha kupelekwa kwa kombora la kwanza ilikataa kutoa maoni yake juu ya habari za hivi karibuni kwamba makombora mengine yamesafirishwa Mashariki mwa pwani ya nchi hiyo.
Vitisho hivyo vya Korea kaskazini ni mojawapo ya misururu ya vitisho vya wiki kadhaa sasa, kufuatia vikwazo vya Umoja Wa Mataifa dhidi yake na mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea kusini.
Marekani yatoa maoni yake
Huku hayo yakiarifiwa Marekani imesema itaweka mizinga ya kujikinga na makombora katika kisiwa chake cha Pasifiki cha Guam kuimarisha uwepo wake wa kijeshi katika eneo hilo.
Hata hivyo wachambuzi wengi wanaofuatilia swala hili kwa makini wanasema Korea Kaskazini haina uwezo wa kuishambulia Marekani.
Tangu vitisho kuanza kutolewa kumekuwa na fununu kwamba mashambulizi hayo huenda yakafanyika siku ya kuzaliwa kwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, hayati Kim Il-Sung, ambayo ni katikati ya mwezi wa Aprili.
Ban Ki Moon aisihi Korea Kaskazini kusimamisha vitisho
Vitisho hivyo vya mara kwa mara kutoka Korea Kaskazini kwa Marekani vimezua hisia mbali mbali miongoni mwa jamii ya kimataifa.
Kwa upande wake katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akisema kwamba vitisho vya aina hiyo vinatia hofu na huenda vikasababisha athari kubwa.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon.
Alisema Ban Ki Moon.
Hapo jana Korea kaskazini iliwazuia wafanyikazi kutoka Korea kusini kuingia katika kiwanda cha Keosong.
Hatua hiyo inalenga kuwasimamisha kazi wafanyakazi takriban 53,000 kutoka Korea Kusini. http://www.dw.de
0 comments:
Post a Comment