Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb)
akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa
Fedha 2012/2013 na mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
Wizara kwa mwaka wa Fedha 2013/2014 kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani)
inayoongozwa na Mhe. Edward N. Lowassa (Mb.) (kulia). Kikao hicho
kilifanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam tarehe 3
Aprili, 2013.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma
Maalim (Mb.) (kulia-mstari wa kwanza), akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo
pichani) wakati wa kikao kati ya Uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge ya
Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Wengine katika
picha ni Bw. John Haule (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Rajabu Gamaha (kushoto), Naibu
Katibu Mkuu.
Baadhi
ya Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe
(hayupo pichani).
Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wengine wa Kamati hiyo wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Wakurugenzi wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani).
Baadhi
ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe
(hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya Uongozi wa Wizara na Kamati ya
Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wakurugenzi
na Wajumbe wengine kutoka Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Waziri Membe (hayupo
pichani) wakati wa kikao kati ya uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Picha Zote na Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiani wa Kimataifa
0 comments:
Post a Comment