BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAKOMBORA YA KINANA, ADAI CHADEMA KIMEPANIA KUIVURUGA NCHI.

Kwa ufupi

“Nataka muelewe, hawa wanasema people’s power bila kufahamu kuwa nguvu ya umma inapatikana kwenye masanduku ya kura, Abdulrahman Kinana.Baadhi ya wananchi waliofika kwenye Uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege, Morogoro kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara kuhitimisha ziara yake ya siku nane mkoani humo jana. Picha Juma Mtanda. 
Mbunge wa Morogoro Mjini Abdulaziz Abood alisema kazi yake siyo kutunisha misuli bungeni bali kuwatumikia wananchi.

MOROGORO. 
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amehitimisha ziara ya siku nane mkoani wa Morogoro kwa kukishambulia Chadema akisema kimepania kuivuruga nchi.

Katika ziara hiyo ya kukagua na kuimarisha uhai wa CCM mkoani humo, Kinana alisema hiyo inatokana na kauli mbalimbali alizoziita ni za kukatisha tamaa.

Akihutubia mamia ya wananchi kwenye Viwanja vya Fire nje kidogo ya Mji wa Morogoro, Kinana alisema Chadema ni moja ya vyama visivyokubalika kwa kuwa hakikubaliani na kila kinachofanywa na Serikali ya chama chake.

“Wananchi msikubali kuongozwa na watu wasiokubali maendeleo... Tumejenga hospitali, wanasema hakuna kitu, tumejenga barabara hawataki, tumetimiza ahadi za maji katika maeneo mengi hawataki, kila kitu hawataki sasa hawa ni watu wa namna gani? Akili za kuambiwa, changanya na zako.

“Kumekuwa na mpangilio wa mchakato wa Katiba, wao wanasema haufai, muda uliowekwa hautoshi, wajumbe wa mchakato ni mbumbumbu, utaratibu uliowekwa ni wa ovyo na hawana weledi, sasa wanataka kitu gani !.

“Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba alizungumza na waandishi wa habari mchakato mzima ili wananchi wafahamu, Rais Jakaya Kikwete alizungumza tena yaleyale katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, wakasema aaah! Wamepora mchakato mzima hatukubali.


“Tutaitisha maandamano nchi nzima kupinga mchakato. 

Sasa kueleza imekuwa makosa? Ninawaomba wananchi kuwa macho na hawa watu kwani dhana yao kubwa ni kuona nchi yetu haitawaliki na Rais ameshasema, akili za kuambiwa, changanya na zako.

“Nataka muelewe, hawa wanasema people’s power bila kufahamu kuwa nguvu ya umma inapatikana kwenye masanduku ya kura, ninawaomba wananchi mjihadhari na Chadema kwa kuwa viongozi wake ni wabinafsi, wenye uchu wa madaraka na siku zote ndoto zao ni kuingia ikulu.

“Nina mambo matatu nataka kuwaambia Chadema, kwanza; wajue hawako peke yao katika maendeleo ya nchi. Tuko wengi na wote tunahitaji kuona kunakuwapo na maendeleo wanaposema wanaleta maendeleo, yapi ?.

“Pili; wameachiwa muda mrefu na hata kujenga kiburi, sasa Watanzania wakatae hoja zao na ninasema Watanzania wakatae maneno yao ya uongo kuwa Serikali ya CCM haikufanya lolote, wewe kama unaona hakuna maji, ihoji Serikali, kama hakuna barabara ihoji Serikali...

“Tatu; wakubali kuwa Katiba si ya CCM wala CUF wala, TLP, Wala Chadema ni ya wote. Kila Mtanzania amepewa nafasi kuijadili na kutoa maoni yake, hakuna chama kilichohodhi mchakato wa Katiba... 

Ninawashangaa hawa na ninawaambia Watanzania na wabunge wa CCM tembeeni kifua mbele, msiogope hoja zao.”
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: