Akizungumza
na waandishi wa habari hii jana katika ofisi ya CHADEMA mkoa mbunge wa
Arusha mjini Godbless Lema ameelezea nia yake ya kumshitaki, Magesa
Mulongo kwa kumtumia ujumbe wa matisho katika simu yake ya mkononi.
Ameeleza
kuwa Mulongo ametumia kila njia kutafuta simu yake ikiwa ni pamoja na
kutaka kumrubuni mke wake na pia kumtumia Mbunge wa Arumeru Mashariki
kuzungumza nao ili simu iyo iwasilishwe polisi ila imeshindikana.
'Wanasheria
wangu wapo katika hatua za mwisho kuandaa mashitaka dhidi ya Mulongo'
amedai kamanda Lema..miongoni mwa mawakili wa Lema atakuwepo Kamanda
Tundu Lissu
0 comments:
Post a Comment