BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MADEREVA KUPIMWA KILEVI, WATAOBAINIKA KUFUTIWA LESENI NCHINI.

Kwa ufupi“Ndiyo maana Sumatra tumeamua kuanza kuchukua hatua za kutoa vifaa vya kupima madereva walevi ili kupunguza ajali za barabarani,” alisema.http://www.mwananchi.co.tz. Inspekta Jenerali Mwema.
 
DAR ES SALAAM. 
KIKOSI cha Usalama Barabarani cha Jeshi la Polisi kitaanza kuwapima madereva kilevi na watakaothibitika kulewa huku wakiendesha magari watanyang’anywa leseni na kushtakiwa.Uamuzi huo unalenga kupunguza ajali za barabarani ambazo zimezidi kuongezeka siku hadi siku.
Hatua hiyo imekuja baada Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kufanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 76 ya ajali zinasababishwa na makosa ya binadamu.

Kaimu Mkurugenzi wa Sumatra, Ahmed Kilima alisema hayo jana alipokuwa akikabidhi vifaa vyenye thamani ya Sh13 milioni kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema ambavyo vitatumika kupimia kilevi kwa madereva. 


Takwimu za Kikosi cha Usalama Barabarani zinaonyesha kwamba kulikuwa na vifo 1,808 vilivyotokana na ajali 11,163 kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu wakati katika kipindi hichohicho kwa mwaka 2011, kulitokea ajali 1,763.

Kilima alisema utafiti uliofanywa mwaka 2007 ulibaini kwamba asilimia 76 za ajali za barabarani zilisababishwa na makosa ya binadamu, asilimia 16 ubovu wa magari na asilimia nane barabara mbovu. 


Kilima alisema ulevi kwa madereva ni miongoni mwa makosa ya kibinadamu ambayo yameainishwa katika utafiti huo.

“Ndiyo maana Sumatra tumeamua kuanza kuchukua hatua za kutoa vifaa vya kupima madereva walevi ili kupunguza ajali za barabarani,” alisema.

Alisema madereva watakaobainika kutumia kilevi wakati wanaendesha vyombo vya usafiri watashtakiwa pamoja na kunyang’anywa leseni zao ili wasifanye kazi hiyo tena.


“Tunawatahadharisha madereva kuacha kabisa pombe wakati wakiwa kazini vinginevyo watazuiwa kufanya kazi hiyo. Wachague udereva au pombe kwa kuwa vitu hivyo haviwezi kufanya kazi pamoja, tunafanya hivi ili kupunguza maafa,” alisema.

Kwa upande wake, Inspekta Jenerali Mwema alisema madereva hasa wa daladala wamekuwa wakitumia pombe kali wakati wakiendesha magari.

“Kuna pombe kali zinauzwa kwenye vituo vya daladala, wanazinunua na kuziweka kwenye chupa za maji, vifaa hivi vitawaumbua na tutawakamata,” alisema Mwema.


Alisema vifaa hivyo vitasaidia kuzuia ajali kabla hazijatokea kwa kuwa vinawabaini walevi kabla hawajasababisha ajali.

Mwema alisema kuanzia sasa jeshi hilo litasambaza namba za simu za makamanda wa mikoa na maofisa wa polisi wa wilaya ili wananchi waweze kuwasiliana nao kila linapotokea tatizo.


“Ukisafiri popote Tanzania utakuwa na namba ya polisi kulingana na mahali ulipo. Itakusaidia kutoa taarifa kila unapoona tatizo la kihalifu au makosa ya barabarani,” alidokeza Mwema.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: