BI KIDUDE AKIPIGA NGOMA ENZI ZA UHAI WAKE.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Mohamed Shein, wakishiriki katika
dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika
mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini Zanzibar. Bi Kidude
anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati,
Unguja.Picha na OMR
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Ramadhan Nasib (kulia)'Diamond Plutnum',
akiwa ni mmoja kati ya wasanii waliohudhuria katika dua maalum ya
kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu
katika Msikiti wa Mwembeshauri, mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia
kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja. Picha
na OMR.
Waumini
wa dini ya Kiislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Fatma
Baraka 'Bi Kidude'(picha ndogo juu kushoto), wakati wakiingiza jeneza
hilo Msikiti wa Mwembeshauri, kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea
kijijini kwa marehemu, Kitumba Wilaya ya Kati kwa maziko, mchana huu.
Picha na OMR
0 comments:
Post a Comment