Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) na
Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Beatrice Shelukindo, kwa pamoja
wakipokea nishani kwa niaba ya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, kutoka
kwa Dkt. Mohammed Zaharani (katikati yao) kwa wa kwanza (kulia) ni
Haruna Mbeyu maarufu kama Meya wa London na anaefuatia ni, Mariam
Mungula , Katibu wa Tanzania Women Association (TAWA) UK.
Baadhi
ya Akina Mama waKitanzania waliohudhuria hafla hiyo katika picha ya
upendeleo na Mhe. Beatrice Shelukindo na Nishati ya Mama Salma .
Akina Mama hao walitamani wote wapande ndege kuelekea jijini Dar Tanzania ili kuikabidhi Nishani hiyo .
****************************
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete, ambaye
pia ni Mwanaharakati wa Kijamii kupitia Chama Chake cha Wanawake na
Maendeleleo, na Taasisi ya WAMA, wiki iliyopita alizawadiwa Nishani na
Chama kinachojishughulisha na kuinua kiwango cha Elimu kwa Nchi za
Afrika Mashariki kilichopo jijini London, Uingereza.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyikia katika kumbi za Hoteli ya Park
Plaza iliyopo pembeni mwa Westminster Bridge (katikati ya jiji la
London) Dkt. Mohammed Zaharan, ambaye ni Katibu wa Chama hicho cha East
Africa Education Foundation (EAEF) alisema kuwa Chama Chake kimekuwa
kikifuatilia kwa ukaribu shughuli zinazofanywa na Mama Kikwete kupitia
Jumuiya ya WAMA ambapo wamefurahishwa na utaratibu wa TAASISI hiyo na
kuamua kuitunuku Nishani.
''Tumepata
fursa hii ya kumtunukia "Award" kwa kutambua mchango wake mkubwa sana
wa kuinua Elimu ya Mtoto, hususan wa kike na vilevile kuwezesha Wanawake
ili waweze kujitegemea''. alisema Dkt Zaharani
Aidha
Dkt. Zaharani aliongeza kuwa Mama Kikwete ni mfano bora sana wa kuigwa
na Wanawake wengine katika jamii ndani na nje ya Tanzania.
Akipokea
Nishani hiyo kwa Niaba ya Mama Salma Kikwete, Naibu Spika Mh. Job
Ndugai, aliyekuwa Nchini Uingereza kwa Mualiko wa Naibu Spika wa
Uingereza na aliyeongozana na Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya
Utumishi ya Bunge, alisema kuwa amefurahishwa sana na kitendo hicho cha
Mchango wa Mama Salma kuonekana, kwa kuwa kinadhihirisha mchango
unaofanywa na Jumuiya zisizo za Kiserikali katika jamii kama WAMA
unaonekana mpaka Nje ya Tanzania.
Naye
Mhe. Mama Beatrice Shelukindo alifurahi zaidi kwa kitendo tukio hilo na
kusema kuwa hili ni jambo kubwa sana na linadhihirisha mchango mkubwa
wa Mama Salma katika kumuendeleza Mwanamke wa Kitanzania na inatia moyo kwa Wanawake Wengine.
HONGERA
SANA MAMA SALMA NA MWENYEZI MUNGU AZIDI KUKUONGOZA NA KUKUPA AFYA NJEMA
ILI UWEZE KUCHANGIA ZAIDI KATIKA MAENDELEO YA MWANAMKE NA MTOTO WA
KIKE.
CREDITS: SUFIANI MAFOTO
0 comments:
Post a Comment