MHE WENJE AWATUSI VIONGOZI WA SERIKALI KATIKA BUNGE DODOMA LEO.
CHANZO http://www.habarimpya.com
Bungeni,Dodoma
BUNGE la Jamhuri wa muungano wa Tanzania limekuwa uwanja wa matusi baada ya wabunge kutoleana Lugha ya matusi na maneno machafu wakati wa kuchangia hutuba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kusababisha kelele kutawala kikao hicho cha bunge.
Baadhi ya wabunge wamesema hivi punde kwamba Wenje amewatukana viongozi wa serikali na huku akiaidiwa kwamba atashungulikiwa.
Naibu Spika, Job Ndungai amesema kwamba atamshugulikia Wenje " Tunawaomba sana waheshimiwa wabunge, hatujaja hapa kutukanana na kuvunjiana heshima.
Tuchunge kauli zetu na kufanya kazi pamoja," amesema Ndugai.
Mbunge wa Iringa Mjini Chadema, Mchungaji Peter Msigwa alitumia Bibilia kunukuu baadhi ya mistari ya kitabu hicho kitakatibu kinachoaminiwa na waumini wa dini ya Kikristo na kudai kwamba 'upumbavu ukiutwanga kwenye kinu hauwezi kwisha' akimaanisha kwamba mtu mpumbavu atabaki kuendelea kuwa mpumbavu.
Msigwa alikuwa akisema kwamba mambo mengi yamekuwa yakifanywa kisiasa na akatolea mfano kwamba mpaka sasa Waziri Mkuu hajafanikiwa kutatua tatizo la udini.
Naye Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekia Wenje ailishambulia serikali akisema kwamba serikali haiko makini katika kushugulikia matatizo yakiwamo ya upungufu wa maji, kudorora kwa elimu na miundombinu.
Ilipofika zamu ya Erasto Zambi (CCM) aliushambulia kambi ya upinzani hasa Msigwa akimwambia kwamba amelidhalilisha ibilia na kwamba maaskofu na waumini wa Kikristo hawapendi kuona Bibilia ikidhalilishwa.
Anna Abdallah CCM amesema kwamba Msigwa amewadhalilisha wanawake kwa kuwaita wapumbavu na kwamba wasikubali kudhalilishwa.
0 comments:
Post a Comment