Na Juma Mtanda, Morogoro.
MOTO mkubwa umezuka katika
bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya wafugaji ya Parakuyo na kusabisha
hasara baada ya moto huo kuteketeza mali mbalimbali za wanafunzi vikiwemo nguo,
madaftari, vitanda na magodoro katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi mjini hapa kwa njia ya simu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya
Kilosa, Ameri Mbaraka alisema kuwa moto huo ulianza majira ya saa 2 usiku wa
April 11 mwaka huu na kuteketeza mali za wanafunzi hao ambapo haukuweza kuleta
madhala kwa binadamu.
Mbaraka alisema athari kubwa
za moto huo ni kutekeza mali zilizokuwemo katika vyumba vya bweni hilo ikiwa ni
pamoja na nguo, madaftari, vitanda na magodoro ambapo wanafunzi hao
walihamishiwa katika vyumba vya madarasa kwa ajili ya kulala huku juhudi za
haraka zikiendelea kufanywa za kuwapatia msaada muhimu.
Msaada ambao unahitajika kwa
sasa ni pamoja na magodoro, madaftari, nguo za kushindia na sare, vitanda
ambapo moto huo ulizuka wakati wanafunzi wakiwa darasani wakijisome. Alisema Mbaraka.
Mbaraka alisema kuwa juhudi
za kuzima moto huo kutoka wa wananchi, walimu na wanafunzi zilishindikana
kutokana na kukosa vifaa vya kuzima moto na kushuhudia mali zikiteketea.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa
halmashauri hivi sasa inajipanga kuona namna ya kusaidia katika janga hilo na
kuweka mikakati ya kuweka vifaa vya kuzima moto katika shule zote za sekondari
za wilaya hiyo.
Naye mmoja wa
wanafunzi wa shule hiyo Zuhura Nuiwai alisema kuwa serikali ione namna ya
kuwapatia msaada wanafunzi hao kutokana na hasara waliyopata kutokana na moto
huo.
Hadi sasa chanzo
za moto huo bado hakijajulikana na taarifa zimeelezwa kuwaa wanafunzi watano
wamepoteza fahamu kwa mstuko kutokana na tukio hilo na wamelezwa katika
hospitali ya Kimamba wilayani humo.
0 comments:
Post a Comment