BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MSTAHIKI MEYA WA ILALA AZINDUA KAMBI YA STARKEY IKIWA NI HUDUMA YA BURE YA VIFAA KWA WENYE MATATIZO YA KUSIKIA JIJINI DAR ES SALAAM.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akilakiwa na uongozi wa Starkey alipowasili katika shule ya Buguruni Viziwi kuzindua kambi ya Starkey itakayokuwa inatoa huduma ya uchunguzi, vifaa na matibabu bure kwa wananchi wenye matatizo ya kusikia.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo na mmoja wa wauguzi katika kambi hiyo mara baada ya kuwasili.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akifanyiwa uchunguzi wa tatizo la kutosikia wakati kuzindua kambi ya Starkey itakayosaidia kutoa huduma na matibabu bure kwa wananchi wenye matatizo ya kusikia iliyopo kwenye shule ya watoto wenye ulemavu wa kusikia (Buguruni viziwi) jijini Dar.
 
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh.Jerry Silaa jana tarehe 16 April 2013 amezindua kambi ya Starkey ya kusaidia wananchi wenye matatizo ya kusikia iliyofanyika katika shule ya watoto wenye ulemavu wa kusikia (Buguruni viziwi), ambapo wenye magonjwa watatibiwa na wenye kuhitaji vifaa vya kuongezea usikivu watatengenezewa kulingana na size zao na watapewa bure.
 
Mstahiki Meya amepima na kwa kuwa ameonekana kutokuwa na tatizo amepata fursa ya kutengenezewa “custom made earphones” wote wenye matatizo mnakaribishwa. Huduma hii ni bureee…
Picha juu na chini ni Mstahiki Meya Jerry Silaa akivishwa “Custom made earphones” na mmoja wa madaktari bingwa katika kambi hiyo mara baada ya kuzindua huduma hiyo atakayokuwa ikitolewa bure kwa wananchi wenye matatizo ya kusikia.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akimsalimia mmoja wa watoto waliofika kambini hapo kupatiwa huduma baada ya kuizindua.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo ya namna huduma hiyo itakavyokuwa ikitolewa kwa wagonjwa watakaofika kambini hapo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa kambi hiyo mara baada ya kuzindua.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: