TUNAOMBA RADHI KWA KUWALETEA
TAARIFA NDEFU KIASI HIKI KWANI MNATAMBUA KUWA SERA ZETU NI KUTOA TAARIFA
KWA UFUPI TU, LAKINI KUTOKANA NA UNYAMA, UKATAILI ALIOFANYIKA MTOTO
HUYU,HABARIMPYA.COM IMEAMUA KUWALETEA TAARIFA HII KWA UNDANI ZAIDI HIVYO
TUNAOMBA UISOME KWA UMAKINI MKUBWA MWANZO HADI MWISHO.
UKICHOKA PUMZIKA NA URUDI BAADAYE KWANI ITAENDELEA KUWA HAPA KWA ZAIDI YA WIKI NZIMA BILA KUPOTEA.HABARIMPYA.COM PIA INALAANI TUKIO HILI KWA NGUVU ZOTE, TUNAOMBA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE ILI IWE FUNDISHO KWA WATU WENYE TABIA ZA AINA HII, MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMEN.
Marehemu Debora Riziki miaka 3 enzi za uhai wake
Riziki Mwangoka kulia anaetuhumiwa kumzika mtoto wake akiwa hai
Hapa maiti ya mtoto Debora ikiwa imetolewa nnje mara baada ya kufukuliwa ndani ya nyumba ya baba yake mzazi
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI TUNAZOZIONYESHA
Mwili wa marehemu Debora ukionyeshwa kwa mzazi na kudhibitisha kuwa ndiye mwenyewe aliyemfukia
Mwili wa mtoto Debora ukiandaliwa kwa kuzikwa kwa heshima zote
Mwili wa Debora tayari kwa kuzikwa
Hatimae sasa Debora anazikwa
Mara tu baada ya mazishi baba mzazi wa Debora anapelewa kituo cha polisi Tukuyu
Mama mzazi wa marehemu Debora asimulia kisa chote
Mama mzazi wa Marehemu, Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili
Bibi wa marehemu Debora
Tukiwa na baadhi ya waandishi wenzangu tukiendelea kupata historia fupi ya marehemu Debora toka kwa mama yake mzazi
Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake, walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha miaka saba.
Dada wa marehemu Debora, Neema Stevini(5) kulia ambaye ni
mtoto wa kufikia wa baba mzazi wa marehemu, akisimulia jinsi mdogo wake
alivyoibwa , alisema kuwa anakumbuka mara ya mwisho ilikuwa jioni majira
ya saa 12 jioni.
“Nilitaka kwenda nao, lakini baba
Debora akaniambia nirudi kuchochea moto ndani na niliporudi nikakuta
wameondoka na nilipokimbilia sana siku waona” alisema kwa masikitiko
Neema.
MKASA wa baba kumuua mwanae kwa
kumzika akiwa hai kutokana na mgogoro wa ndoa, umezidi kuibua mapya,
baada ya mama mzazi wa marehemu ,Debora Riziki (3), kusimulia mkasa
mzima .
Akizungumza kwa hisia kali,
katika mahojiano maalumu na Mbeya yetu kijijini kwake Ibula, katika
kata ya Kiwira, wilayani Rungwe, Mama mzazi wa Marehemu, Esther
Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na viashiria
vingi vya mumewe kufanya ukatili.
Alisema tukio la mzazi mwenza
huyo kumwiba mtoto na kwenda kumfanyia ukatili huo wa kinyama lilikuwa
la pili, baada ya awali kumuiba akiwa na miaka miwili na miezi mine na
alimrudisha kwa maandishi ya serikali ya kijiji.
Alisema katika tukio la kwanza la
mtalaka wake huyo kumuiba mtoto wao huyo, lilitokea Septemba mwaka
2012, baada ya wiki chache za kumfukuza katika nyumba waliyokuwa
wakiishi katika kitongoji cha Iponjola, kijiji cha Asenga, nyumba
iliyotumika kuzikwa mtoto huyo.
Alitaja sababu za yeye kufukuzwa
ni ugomvi uliotokana na yeye kuhoji sababu za kuficha fedha kiasi cha
sh. 120,000 zilizotokana na wao kwa pamoja kufanya kazi ya kibarua
katika mashamba kijijini hapo na baada ya malipo kutolewa mtalaka wake
huyo alionesha kiasi kidogo cha sh.80,000.
Alisema ugomvi huo ndio
ulisababisha yeye arudishwe kwa wazazi wake, lakini baada ya muda mfupi
mwanaume huyo alimfuata na kumbembeleza ili warudiane na alipogoma
aling’ang’ania aondoke na mtoto .
“Nakumbuka ilikuwa Novemba mwaka
jana baada ya mimi kuondoka nyumbani kwake na kurudi kuishi hapa
nyumbani, siku hiyo tukiwa shambani huyo bwana alikuja hapa nyumbani na
kumkuta mwanangu wa kwanza (Neema Steven ) niliyezaa na mwanaume
mwingine” alisema Mwambenja.
Alisema baada ya kufika eneo hilo
majira ya saa mbili asubuhi alitumia ujanja na kufanikiwa kumuiba mtoto
na kisha kutokomea naye kijijini kwao Asenga, hali ambayo ilisababisha
kutoa taarifa kituo cha polisi Kiwira.
“Unajua kuwa baada ya kwenda
kutoa taarifa polisi walitusaidia kufika kijijini kwao ambapo serikali
ya kijiji ilikubali nimchukue mwanangu kwa kuwekeana mkataba wa kisheria
kwa mujibu wa sheria, kwani alikuwa chini ya miaka saba”.
Aliongeza kuwa Novemba 15 mwaka
2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na
mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake, walinikabidhi barua ya
kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya mume wangu kutorudia kosa
hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha miaka saba.
Tukio la pili la kuiba mtoto.
Alisema tukio hilo lilitokea
Novemba 29 mwaka jana 2012, ambapo alifika nyumbani kwao majira ya saa
12 :00 na kumkuta dada wa marehemu kumchukua mtoto akimdanga kuwa
anaenda kusenya kuni eneo la jirani.
Aliongeza kuwa baada ya kuona
dada wa marehemu anang’ang’ania kwenda wote alimuamuru arudi nyumbani
kuchochea moto kwa kuwa kulikuwa kumeinjikwa mboga na kukubali kurudi.
“kwa mujibu wa maelezo ya
mwanangu huyu wa kwanza alisema baada kurudi toka ndani, alikuta baba
yake huyo ameondoka na mtoto na tuliporudi na kupokea taarifa hizo
tulichanganyikiwa na kuanza kuhangaika hovyo” alisema mama wa marehemu.
Mwambenja alisema kuwa baada ya
kucha siku ya pili asubuhi yake walienda kutoa taarifa kituo cha polisi
cha Kiwira ili waweze kupata msaada wa kumtafuta, huku wakionesha barua
ya makubaliano ya awali ya yeye kuwa na haki ya kisheria ya kusimamia
malezi ya mwanao hadi afikishe miaka saba.
Alisema baada ya kutoa taarifa
hizo kituoni hapo, askari aliyekuwa zamu siku hiyo alimtaka kutoa kiasi
cha shilingi 50,000 ili fedha hizo wapewe askari mgambo wa kwenda
kijijini kwa mzazi mwenzake huyo, kwani tayari walikuwa na taarifa kuwa
alikuwa amekimbilia huko.
“Kutokana na hali ngumu ya
maisha tulikosa kiasi hicho cha fedha hivyo suala hilo kubaki bila
msaada wa polisi na pia hatukuweza kwenda kwa kijijini kwao”.
Aliongeza “sababu ya mimi kuwa
mzito kuendelea kumfuatilia kijijini kwao kwa mara ya pili ili kujua
kama yupo huko na mtoto ilitokana na hofu niliyoijenga, kwani awali
tukiwa kwenye ugomvi alitamka maneno ya vitisho kuwa endapo nitaendelea
kung’ang’ania kumchukua mtoto pale anapomchukua atakuja kumuua ili
tukose wote”.
Hata hivyo mama huyo mzazi wa
Debora, alisema kuwa baada ya kuona hali hiyo, aliendelea kuwasiliana na
wifi yake , Bupe Mwangoka,ambaye ni dada mkubwa wa mume wake anayeishi
eneo la Isanga Jijini mbeya, ambaye ndiye alisaidia kwa kiasi kikubwa
kubainika kwa unyama aliofanya.
Maisha kabla ya tukio.
Akielezea maisha yao kabla ya
kutengana na baadae kuamua kufanya ukatili huo, alisema aliwahi
kumtamkia maneno makali wakati akiwa na ujauzito wa miezi nane .
Alisema baada ya kuibuka ugomvi
katika kipindi hicho, mwanaume huyo alimtaka kwenda kuiuza mimba ile kwa
mwanaume mwingine yeyote atakayempenda ili asije akazaa mtoto ambaye
atachanganya damu ya koo hizo mbili.
“Maneno yale katika kipindi hicho
sikuyatilia maanani kwani nilifikiri zilikuwa ni hasira, lakini leo hii
ndio najua maana ya ile kauli ” alisisitiza Mwambenja.
Hata hivyo alisema inashangaza
kwani kuna wakati tukiwa katika maisha ya kawaida kabla ya yeye kufanya
tukio hilo, mara kadhaa alijutia na kuonya juu ya matukio machafu
yaliyojitokeza na kusikika ya watu kuuawa au kuondolewa baadhi ya viungo
vya miili yao.
Aidha, alieleza mkasa mwingine wa
mume wake huyo ni ule wa wao kufukuzwa katika mji wa Kiwira walikokuwa
wakiishi awali kwa kufanya shughuli za umachinga.
Alisema walitimuliwa na serikali
ya mtaa katika mji huo kutokana na mumewe huyo kutuhumiwa kuiba simu ya
mkononi ambapo alipokea kipigo kikali na baadae kufukuzwa.
Kutokana na hali hiyo, mama wa
marehemu Debora alisema yote yaliyotokea amemwachia mungu na kwamba kama
ingekuwa uwezo wake angeamuru naye anyongwe, hivyo mamlaka husika
zitajua cha kufanya.
Kwa upande wake dada wa marehemu
Debora, Neema Stevini(5) ambaye ni mtoto wa kufikia wa baba mzazi wa
marehemu, akisimulia jinsi mdogo wake alivyoibwa , alisema kuwa
anakumbaka mara ya mwisho ilikuwa jioni majira ya saa 12 jioni.
“Nilitaka kwenda nao, lakini baba
Debora akaniambia nirudi kuchochea moto ndani na niliporudi nikakuta
wameondoka na nilipokimbilia sana siku waona” alisema kwa masikitiko
Neema.
Hata hivyo uchunguzi wa Mbeya
yetu umebaini kuwa marehemu Debora alifariki dunia siku hiyo ya Novemba
29 mwaka jana, majira ya saa nne usiku baada ya baba yake kufanikiwa
kumuiba kutoka nyumbani kwa mama yake.
Inadaiwa kuwa baada ya kufanikiwa
kumtorosha baba huyo wa marehemu alitembea kwa mguu umbali wa kilomita
50 kutoka kijiji cha Ibula alikomuiba hadi nyumbani kwake kijiji cha
Isange katika kata ya Isange.
Imeelezwa kuwa
baada ya kufika nyumbani kwake, baba huyo mzazi wa marehemu alichimba
shimo katikati ya sebule na kumchukua mtoto wake huyo akiwa usingizini
na kisha kumfukia akiwa hai.
Mwanaume Yule alikuwa katili
sana, kwani baada ya kumfukia alichukua meza ya chakula na kuiweka juu
yake huku akiipamba kwa magazeti jambo ambalo lilifanya ndugu zake
wasigundue kirahisi” alisema mpasha habari.
Chanzo hicho kilisema baada ya
kufanya hivyo aliishi kwa wiki moja na baadae kukimbilia Jijini Mbeya
ili watu wasibaini juu kitendo alichofanya na kwamba kila alipohojiwa na
ndugu zake alisema mwanae huyo alimuweka kwa rafiki yake Jijini Mbeya.
Hata hivyo baada ya danadana za
muda mrefu ndipo dada wa mtuhumiwa huyo aliamua kutoa taarifa jeshi la
polisi na kufanikiwa kumkamata akiwa katika harakati za kutorokea
wilayani Chunya na alipobanwa alifichua siri ya alipo mwanae kwa kueleza
kuwa alimuua na kumfukia ndani kwake.
chanzo habari mpasuko
0 comments:
Post a Comment