Mtuhumiwa wa Mauaji ya Padri
Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Minara Miwili mjini Zanzibar, Omar
Mussa Makame (35) akiwa chini ya ulinzi wakati akielekea chumba cha Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kesi yake
kutajwa mahakamani hapo.
Mtuhumiwa wa Mauaji ya Padri Evarist Mushi wa
Kanisa Katoliki Parokia ya Minara Miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35)
akiwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kesi yake kutajwa mahakamani
hapo.
Mawakili
wanaomtetea Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri , Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki
parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) wakili Abdalla
Juma (kulia) na Rajab Abdalla wakipitia majalada kabla ya kutajwa kwa kesi ya
mteja wao katika mahakama Kuu Vuga mjini Zanzibar. Picha zote kwa hisani ya Francis Dande.
ZANZIBAR.
MTUHUMIWA wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi, Omar Mussa Makame (35) mkazi wa Mwanakwerekwe mjini hapa amefikishwa Mahakama Kuu kwa tuhuma za mauaji ya kiongozi huyo wa dini.
MTUHUMIWA wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi, Omar Mussa Makame (35) mkazi wa Mwanakwerekwe mjini hapa amefikishwa Mahakama Kuu kwa tuhuma za mauaji ya kiongozi huyo wa dini.
Makame aliyegombea ujumbe wa Baraza la Wawakilishi
kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Jimbo la Rahaleo mwaka 2010
alifikishwa mbele ya Jaji Mkusa Sepetu jana.
Awali mtuhumiwa huyo alikuwa afikishwe mahakamani
Jumanne iliyopita, lakini ilishindikana baada ya ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashitaka (DPP) Zanzibar kuinyima kibali Polisi kumfikisha mahakamani.
Haikujulikana sababu ya uamuzi huo kwani
Mkurugenzi wa Mashtaka, Ibrahim Mzee Ibrahim na Kamishna wa Polisi
Zanzibar, Mussa Ali Mussa walitupiana mpira kila mmoja akitaka mwenzake
ndiye ataje sababu hizo.
Viongozi hao wote jana hawakupatikana kueleza
hatua hii mpya ya kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo imekuja baada ya
uamuzi wa aina gani.
Wakili wa Serikali, Abdallah Issa Mgongo alidai
mbele ya Jaji Sepetu kuwa mshtakiwa aliua kwa makusudi Februari 17,
mwaka huu eneo la Beit el Rass Wilaya ya Magharibi Zanzibar.
Mgongo alidai tendo hilo ni kosa kwa mujibu wa vifungu 196 na 197 sheria namba (6) za mwaka 2004 ya sheria za Zanzibar.
“Omar Mussa Makame unashitakiwa kwa kosa la kumuua
kwa makusudi Padre Evarist Mushi siku ya tarehe 17/02/2013 mnamo saa
12:50 za asubuhi,” alidai Wakili Mgongo.
Makame alikataa kosa hilo la mauaji na wakili wa
Serikali aliiomba Mahakama kumrudisha rumande mtuhumiwa hadi hapo
ushahidi utakapokamilika.
Upande wa utetezi wakili wa kujitegemea, Abdallah
Juma aliiomba Mahakama iamuru ushahidi ukamilike baada ya wiki mbili ili
kesi iweze kusikilizwa.
“Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa
ni kwamba ushahidi umekamilika nashangaa leo (jana) wakili wa Serikali
anasema kwamba bado haujakamilika,” alidai Juma.
Baada ya maombi hayo, Jaji Sepetu alikubaliana na
upande wa utetezi na kuwataka mawakili wa Serikali kuharakisha kupeleka
ushahidi ili kesi ianze kusikilizwa. Kesi hiyo imepangwa Aprili 18,
mwaka huu katika mahakama hiyo.
0 comments:
Post a Comment