Kwa ufupi
Utafiti huo wa Machi 23 mwaka huu, ulibaini kwamba
Uganda inaongoza kwa kunywa pombe chafu maarufu kama Luwombo kwa
asilimia 14.52 ikifuatiwa na Rwanda kwa asilimia 6.44.
http://www.mwananchi.co.tzPombe ya kienyeji ikiandaliwa tayari kupelekwa kwa walaji
UTAFITI wa Kituo cha Habari cha Marekani CNN, umebaini kwamba
Tanzania ni nchi ya sita barani Afrika kwa watu wake kunywa pombe chafu
(mataputapu).
Utafiti huo wa Machi 23 mwaka huu, ulibaini kwamba
Uganda inaongoza kwa kunywa pombe chafu maarufu kama Luwombo kwa
asilimia 14.52 ikifuatiwa na Rwanda kwa asilimia 6.44.
Kwa mujibu wa utafiti huo, Tanzania inashika
nafasi ya tano kwa kuwa na asilimia 4.52, ikiwa nyuma ya Burundi yenye
asilimia 5.07.
Ivory Coast imekuwa nyuma ya Tanzania kwa kuwa
asilimia 3.55 huku Tanzania ikiipiku Burkina Faso iliyoambulia asilimia
3.77, kwa wa watu wake kunywa pombe chafu.
Ripoti ya utafiti huo ilisema asilimia kubwa
katika nchi za Afrika, wanapenda kutumia pombe kali kwa lengo la kuondoa
msongo wa mawazo.
Mtaalamu wa masuala ya afya katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha Figo, Dk Francis Fulia aliwataka
wananchi waache kunywa pombe hizo kwa sababu zinatengenezwa katika
mazingira ambayo si salama.
Alisema hali hiyo inahatarisha usalama wa afya zao.
“Watanzania waachane na matumizi ya pombe hizo kwa
kuwa zinatengenezwa katika njia sizisokuwa salama, pia zinasababisha
magonjwa mbalimbali kama figo, ini, moyo ,kupata upofu ama kupoteza
maisha,” alisisitiza.
Dk Fulia pia alipinga juu matumizi ya pombe katika kuondoa msongo wa mawazo.
“Pombe haina uhusiano wowote katika kupunguza
mawazo, inatumika katika kumsahaulisha mtu tatizo lake kwa kipindi
kifupi” alisema.
Aliongeza kuwa njia salama ya kuepuka msongo wa
mawazo ni kusuluhisha kwa kutafuta chanzo cha msongo huo au kupata
ushauri nasaha kutoka katika vituo mbalimbali vya afya.
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na matukio
ya wananchi kujitumbukiza katika unywaji pombe uliokithiri ikiwamo
kunywa pombe aina ya virobo gongo na pombe nyingine.
0 comments:
Post a Comment